Klabu ya soka ya Newcastle ya nchini Uingereza jana Oktoba 7, 2021 imekamilisha dili la kuuza hisa zake katika kampuni la Saudi Arabia Public Investment Fund zenye thamani ya shilingi 9.3 Tilioni . Anaripoti Damas Ndelema Tudarco (endelea)
Klabu hiyo iliokua chini ya tajiri Mike Ashley imefikia makubaliano hayo siku ya jana na kufanikisha dili hilo lenye thamani ya shilingi pauni milioni 300 hiyo ni kutokana na kupitia changamoto nyingi ya ukamilishwaji yake ambao ulianza kabla ya kuanza kwa msimu mpya wa Ligi Kuu Uingeleza na hivyo jana kufikia tamati
Matajiri hao wa klabu ya Newcastle United wana utajiri mkubwa ambao ni mara 10 ya utajiri wa matajiri wa Manchester City Sheikh Mansour Bin Zayed na hivyo klabu hiyo inakua klabu ya kwanza yenye pesa nyingi barani ulaya
Aidha jambo hili lilikua likisubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki na wapenzi wengi wa klabu hii kwani baada ya jana kuamilika kwa dili hili waliandamana mpaka kwenye makao makuu ya klabu yao na kuelekea kwenye uwanja wao wa St james park wakiwa na furaha isiyo na kifani
Orodha ya vilabu matajiri Barani Ulaya kwa sasa 1. Newcastle united E 320b, 2.PSG _ E 220b, 3.Manchester City -23 b, 4.Rb leipzing & salzburg-15.7b, 6.Juventus_ 14b, 7.Chelsea-10.5, 8.La Galaxy- 8b, 9. Arsenal – 6.8 b, 10.Inter Milan – 6.2b
Leave a comment