December 1, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Newcastle yaachana na kocha wake

Spread the love

 

Klabu ya soka ya Newcastle United ya nchini Uingeleza imeachana rasmi na aliekuwa kocha wake Steven Bruce, baada ya makubaliano ya pande zote mbili. Anaripoti Damas Ndelema TUDARco….(endelea)

Maamuzi hayo yamekuja siku chache mara baada ya timu hiyo kukamilisha mchakatao wake wa kuuza hisa, zenye thamani ya shilingi 9.3 tilioni, kwenye kampuni Saudi Arabia Public Fund.

Klabu hiyo ipo kwenye mipango ya kutengeneza kikosi chao baada ya kununuliwa kwa pesa kubwa, hivyo imeamua rasmi kuachana na kocha huyo ambaye anaiacha timu ikishika nafasi ya 19 kwenye msimamo mpaka sasa.

Nafasi ya Bruce kwa sasa inachukuliwa na Graeme Jones ambae atakua kama kocha wa muda mpaka pale watakapo tangaza kocha mpya wakuongoza kikosi hicho.

Kulingana na utajiri walionao klabu hiyo, inatabiriwa makubwa kuja kuwa moja ya vilabu vikubwa barani Ulaya. licha ya changamoto inayokutana nazo hivi karibuni kutoka kwa baadhi ya vilabu wakipinga uwekezaji huo.

Matajiri hao wa klabu ya Newcastle United wana utajiri mkubwa ambao ni mara 10 ya utajiri wa matajiri wa Manchester City Sheikh Mansour Bin Zayed  na hivyo klabu hiyo inakua klabu ya kwanza yenye pesa nyingi barani ulaya.

error: Content is protected !!