October 1, 2022

Uhuru hauna Mipaka

New Zealand kufanya tukio la kihistoria leo

Spread the love

KUSHAMBULIWA na kuua wa kwa Waiumini wa Dini ya Kiislam msikitini kumeibua mambo mengi nchini New Zealand ikiwa ni pamoja na kuimarisha mshikamano wa dini zote. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Leo Ijumaa tarehe 22 Machi 2019, Televisheni na Redio ndani ya taifa hilo zitatangaza moja kwa moja adhana, huku wanawake wengi wakitarajia kuvaa vazi la kiislamu la Hijab kama ishara ya kuonesha uzalendo na umoja wa taifa hilo.

Waziri Mkuu wa New Zealand, Jacinda Adern amesema siku ya Ijumaa ambayo ni siku ya ibada kwa waumini wa kiislamu, taifa hilo litakuwa kimya kwa muda wa dakika mbili, wakati adhana ikiadhiniwa kitaifa kupitia televisheni pamoja na redio ya taifa hilo.

Adern amesema, tukio hilo ni ishara ya kuonesha umoja wa taifa hilo, kufuatia tukio baya na la kusikitisha la shambulizi la risasi lililotokea katika misikiti miwili ya Al Noor na Linwood iliyoko katika mji wa Christchurch, lililotokea Ijumaa iliyopita na kusababisha vifo vya waislamu 50.

Taarifa zinaeleza kuwa, Arden ataungana na waombolezaji wengine karibu na msikiti wa Al-Noor ambao ni miongoni mwa miskiti iliyokumbwa na shambulio la risasi Ijumaa iliyopita.

Wanawake wengi nchini New Zealand wametakiwa kuvaa Hijab kuonesha ishara ya kupinga tukio hilo.

Hadi sasa raia wa Australia, Brenton Tarrant amefunguliwa shtaka la mauwaji akiwa mshukiwa mkuu katika tukio hilo. Vile vile, Bunge la New Zealand  limepiga marufuku uuzaji wa silaha za moto.

error: Content is protected !!