Tuesday , 16 April 2024
Home Kitengo Maisha Burudika Netta, Mr Eazi waangusha kolabo kali ‘Playground Politica’
Burudika

Netta, Mr Eazi waangusha kolabo kali ‘Playground Politica’

Spread the love

MSANII maarufu wa muziki wa Pop, Netta amemshirikisha staa mkubwa wa muziki wa Nigeria, Mr Eazi katika ngoma mpya ya Playground Politica ambayo imeshaanza kuwa gumzo kutokana na ubunifu uliotumika, kuanzia kwenye mashairi mpaka kwenye video ya wimbo huo. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea)

Netta ambaye amejipatia umaarufu mkubwa barani Ulaya, ameamua kuja kitofauti katika ngoma hiyo kwa kuchanganya ladha za Pop na Afrobeat ambapo tangu ngoma hiyo ilipoachiwa, mashabiki wamekuwa na maoni mengi kuhusu ubora wake.

Netta ameeleza kwamba ameamua kumshirikisha Mr Eazi katika ngoma hiyo, ikiwa ni hatua yake ya kuenzi maisha yake ya utotoni, aliyoyaishi nchini Nigeria ambapo hata video ya wimbo huo, imefanyikia nchini Nigeria katika mazingira aliyoishi akiwa mtoto.

Mwanadada huyo ambaye alipotoka Nigeria alihamia nchini Israel, anaeleza kwamba ameamua kurudi nchini Nigeria kufanya ngoma hiyo kwa sababu ana historia kubwa na n chi hiyo tangu akiwa mdogo, akikumbuka jinsi alivyokuwa akifurahia maisha ya utotoni akiwa ‘kibonge’ mtukutu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BurudikaMichezo

Kizz Daniel aunguruma na EP mpya ‘Thankz alot’

Spread the loveMKALI wa muziki nchini Nigeria, Kizz Daniel ametoa EP yake...

BurudikaHabari za Siasa

Samia amchangia Professa Jay mil. 50, Chadema, wasanii wamwaga manoti

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amechangia kiasi cha Sh 50 milioni...

Burudika

Piga makofi kwa Mr. Eazi …achomoka na ‘The Evil Genius’

Spread the loveMAKOFI kwa Mr Eazi! Staa wa Afropop, Mr Eazi ameachia...

Burudika

Kishindo cha Afro B katika “Wo wo wo” akiwa na Rich the Kid&Rimzee

Spread the loveSTAA ambaye alitambulishwa na ngoma maarufu, Afrowave ‘Drogba’, Afro B,...

error: Content is protected !!