WAZIRI Mkuu wa nchini Israel, Benjamin Netanyahu amesema atachelewesha sehemu muhimu ya mipango yenye utata ya kurekebisha mfumo wa sheria ambao umefanya hali ya utulivu kurejea nchini huko. Anaripoti Eliabu Kanyika, DSJ kwa msaada wa mtandao … (endelea).
Aliyasema hayo jana Jumatatu usiku tarehe 27 Machi 2023 kuwa atasitisha sheria ili kuzuia mpasuko kati ya watu. Lakini haijulikani ni nini kucheleweshwa kutafanikisha zaidi ya kujipa muda hadi utulivu urejee.
Pia katika matukio ambayo hayajawahi kushuhudiwa, chama kikuu cha wafanyakazi nchini humo kiliitisha mgomo, na Waisrael waliitazama huduma kote zikisitishwa. Uwanja wa ndege, maduka, hospitali na benki kote huduma zilisimamishwa.
Hatua hiyo iliyoratibiwa ilibunuwa kumrudisha Netanyahu kutoka kwenye ukingo wa kusukuma mbele mageuzi mwishoni mwa wiki hii.
Sambamba na hilo ilifuatia maandamano makali baada ya kumfuta kazi waziri wake wa ulinzi ambaye alikuwa amezungumza kupinga mipango hiyo. Kiongozi wa Upinzani Yair Lapid aliuita “mgogoro mkubwa zaidi katika historia ya nchi”.
Serikali ya mrengo wa kulia zaidi ya Israel kuwahi kutokea, inatafuta kuchukua udhibiti madhubuti juu ya kamati inayoteua majaji. Marekebisho hayo yangeipa bunge mamlaka ya kubatilisha maamuzi ya Mahakama ya juu kwa wingi wa kimsingi na yangefanya iwe vigumu kutangaza waziri mkuu asiyefaa kushika wadhifa huo na kuwaondoa mamlakani
Leave a comment