WAZIRI Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyau, ameng’olewa katika wadhifa huo alioushikilia kwa miaka 12, baada ya Bunge kupiga kura za kumuondoa madarakani. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).
Netanyau aliingia madarakani kwa mara ya kwanza 1996 hadi 1999, kisha 2009 alichaguliwa tena kuwa Waziri Mkuu wa Israel, nafasi aliyohudumu hadi jana Jumapili, alipong’olewa.
Jana tarehe 13 Juni 2021, Netanyau aliondolewa madarakani kwa kura za ndiyo 60 kati ya 120 zilizopigwa, ambapo 59 zilipigwa kwa ajili ya kupinga mwanasiasa huyo mkongwe Israel kuondolewa madarakani, huku moja ikiharibika.

Kufuatia hatua hiyo, Bunge hilo lilimchagua mzalendo mwenye mrengo wa kulia, Naftali Bennett, kuwa Waziri Mkuu wa Israel, ambaye ataongoza umoja wa vyama vya siasa nchini humo.
Kwa mujibu wa makubaliano ya vyama hivyo, Bennett, amabaye ni Kiongozi wa Chama cha Yamina, atashikilia wadhifa huo hadi Septemba 2023, kisha Yair Lapid, atachukua madaraka na kuiongoza Israel kwa miaka miwili.
Kwa sasa Netanyau anabaki kuwa Mkuu wa Chama cha Mrengo wa Kulia cha Likud, ambacho kwa sasa kinakuwa chama cha upinzani nchini humo.
Leave a comment