August 15, 2022

Uhuru hauna Mipaka

NEMC latoa msimamo mpya

Spread the love

BARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limeeleza kuwa, waanzilishi wa mradi wowote unaohusisha mazingira ni lazima wapate cheti cha mazingira, anaandika Hamisi Mguta.

Jaffar Chimgege, Mratibu wa Mazingira Kanda ya Mashariki leo amesema kuwa, hatua hiyo inatokana na kifungu cha 17 cha sheria ya mazingira kinachoeleza malengo ya kuanzishwa kwa baraza hilo.

Amesema, mtu yoyote atakayekua na cheti hicho akumbuke kuwa, kinaweza kuondolewa muda wowote na waziri endapo hatafuata sheria au kama ikigundulika matatizo yoyote yaliyo nje ya uwezo.

“Sheria inaonesha wajibu wa kufanyika kwa tathimini ya athari kwa mazingira (TAM) kwa miradi yote iliyoainishwa kwenye mazingira,”amesema.

Amesema kuwa, kwa kuwa sheria hiyo inasema TAM itafanyikakabla ya kugharamia au kuanza kwa mradi hivyo, haitampa kibali au leseni mtu yoyote mwenye mradi kuanza bila ya kupata cheti cha TAM.

Kutokana na hilo, wanaotegemea kuanzisha mradi ni vyema akaanza mchakato wa kupata cheti mapema.

“Baada ya hapo mwekezaji atawajibika kutekeleza kilichopo kwenye cheti,”amesema.

error: Content is protected !!