August 10, 2022

Uhuru hauna Mipaka

‘Neema’ yawashukia wafungwa Dodoma

Spread the love

KANISA la Waadventista Wasabato Dodoma limetoa magodoro pamoja vifaa mbalimbali kwa wafungwa wa gereza la Msalato vyote vikiwa na thamani ya Shilingi milioni mbili, anaandika Dany Tibason.

Akikabidhi msaada huo kwa Peter Maswaga Mkuu wa gereza la Msalato Askofu Joseph Mgwabi wa Kanda ya Mashariki, amesema kanisa limefanya hivyo ili kutimiza maandiko matakatifu.

Askofu Mgwabi alisema kanisa linatambua kuwepo kwa watu wenye uhitaji ikiwa ni pamoja na wale waliopo magerezani na maandiko yanaweka bayana namna ya kuwasaidia watu wote wenye uhitaji bila kujali dini, rangi wala kabila.

“Nilikuwa na njaa ukanilisha, nilikuwa na kiu ukaninywesha, nilikuwa gerezani ukaja kunitembelea na nilikuwa uchi ukanivika. Hivi ndivyo maandiko matakatifu yanavyosema,” ameeleza Askofu.

Jumla ya magodoro 76, viatu aina ya Mitanjee pamoja na vitabu mbalimbali vya kuwajenga wafungwa kiimani vimekabidhiwa huku Mkuu wa gereza la Msalato akisema msaada uliotolewa kwa gereza hilo utawezesha wafungwa kuishi katika mazingira salama.

“Jamii inatakiwa kutambua kuwa, kuwepo gerezani siyo kutostahili kupata haki ya msingi. Katika magereza kuna mafunzo ambayo wafungwa wanapatiwa ikiwemo ujasiriamali, ushonaji na kulima kilimo cha busitani za mboga mboga,” ameeleza

 

error: Content is protected !!