Tuesday , 23 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Neema yafunguliwa kwa wafanyabiashara wa Tanzania-India
Habari Mchanganyiko

Neema yafunguliwa kwa wafanyabiashara wa Tanzania-India

Spread the love

 

NEEMA imefunguliwa kwa wafanyabiashara wa Tanzania na India, baada ya Kampuni ya Silent Ocean, kuzindua Huduma za usafirishaji mizigo katika mataifa hayo mawili kupitia njia ya bahari. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Uzinduzi wa huduma hiyo umefanyika leo Jumanne, jijini Dar es Salaam, na kuhudhuriwa na wafanyabiashara mbalimbali wa Tanzania wanaochukua bidhaa zao India.

Meneja wa Silent Ocean, Mohamed Soloka, amesema wameanzisha huduma hiyo baada ya kupokea maombi kutoka kwa wafanyabiashara, waliolalamikia changamoto ya mizigo yao kutoka India kuchelewa kufika nchini.

Soloka amesema Huduma Yao itawezesha mizigo ya wafanyabiashara kusafiri kutoka jijini Mumbai, India hadi Dares Salaam, Tanzania kwa muda kati ya siku 17 Hadi 25, badala ya miezi mitatu Hadi sita ilivyo sasa.

Mbali na India, Soloka amesema kampuni ya Silent Ocean inamatawi mengine nchini Uturuki, China, Marekani na Falme za Kiarabu (Dubai).

Akizungumza katika uzinduzi huo, mwakilishi wa wafanyabiashara wa Watanzania India, Wahid Abdul, Amesema kabla huduma hiyo haijaanzishwa walikuwa wanakabiliwa na changamoto mbalimbali hususan na mizigo kuchelewa kufika nchini, kitendo kilichopelekea baadhi ya mizigo yao kuharibika au kupitwa na wakati.

“Kwa kipindi kiregu tumekwua tukitumia muda mrefu mizigo kutufikia, kuanzia kununua India mpaka kutufikia Tanzania sababu ilikuwa inachukua miezi mitatu mpaka sita hivyo bidhaa zilikuwa zinatufikia zikiwa zimechoka na huwa nje ya fashion (nje ya wakati),” amesema Abdul.

Katibu wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania, Abdallah Mwinyi, amesema Huduma hiyo itasaidia wafanyabiashara kusafirisha mizigo yao moja kwa moja kutoka jijini Mumbai, India Hadi Dar es Salaam.

“Miaka kumi iliyopita nilikuwa nafanya biashara kutoka India mpaka Tanzania, lakini tulikuwa na changamoto ya mizigo kuchelewa kufika, ilikuwa inachukua miezi mitatu mpaka sita, lakini huduma iliyozinduliwa Leo itatusaidia kuwahisha usafiri kwa siku 17 Hadi 25,” amesema Mwinyi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

NMB yadhamini Mkutano Mkuu ALAT, kufunguliwa na Samia

Spread the loveBENKI ya NMB, imekabidhi hundi yenye thamani ya Sh. 120...

Habari Mchanganyiko

DC ampongeza Dk. Rose Rwakatare kwa kusaidia waathirika wa mafuriko Mlimba

Spread the loveMWENYEKITI wa Wazazi CCM Mkoa wa Morogoro, Dk.  Rose Rwakatare...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mipango na uwekezaji kutumia bilioni 121.3, mradi wa Bagamoyo wapewa kipaumbele

Spread the loveWIZARA ya Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, imeliomba Bunge...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mbunge ataka kasi uzalishaji walimu ipunguzwe akidai hakuna ajira

Spread the loveMBUNGE wa Mlalo (CCM), Rashid Shangazi, ameishauri Serikali ipunguze kasi...

error: Content is protected !!