Wednesday , 24 April 2024
Home Habari Mchanganyiko NEEC, GGML yawajengea uwezo wajasiriamali 500 Geita
Habari Mchanganyiko

NEEC, GGML yawajengea uwezo wajasiriamali 500 Geita

Mkurugenzi Mkuu wa GGML, Richard Jordinson (kushoto)akitoa hotuba kwenyemafunzo hayo ya wafanyabiashara mkoani Geita. Kulia ni Meneja Mahusiano wakampuni hiyo, Joseph Mangilima akitafsiri hotuba hiyo kwa washiriki.
Spread the love

WAJASIRIAMALI 500 Mkoa wa Geita ili wawe na fursa bora ya kufanya biashara na taasisi mbalimbali nchini Tanzania. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Mafunzo hayo yametolewa jana Alhamisi tarehe 19 Novemba 2020 na Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) yaliyoratibiwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC).

Mafunzo hayo ni matokeo ya makubaliano yaliyofikiwa na GGML na NEEC 20 Julai 2020 kuhusu namna bora ya kuwasaidia wajasiriamali mkoani Geita ili wapate fursa bora ya kufanya biashara na taasisi mbalimbali.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa mafunzohayo katika ukumbi wa kituo cha uwekezaji mjini Geita, Mkurugenzi Mtendaji wa GGML, Richard Jordinson alisema, kampuni hiyo inalenga kuboresha ushiriki wa wafanyabiashara mkoani humo katika zabuni mbalimbali zinazotangazwa na kampuni hiyo.

Alisema lengo ni kuwajengea uwezo ili wafahamu vigezo muhimu na kutimiza matakwa ya kisheria kusambaza bidhaa na huduma mbalimbali kwenye sekta ya uchimbaji madini sanjari na sekta zingine.

Aliongeza mafunzo hayo ni uthibitisho tosha kuwa kampuni ya GGML inakusudia kuchochea maendeleo endelevu kwa jamii inayozungukamgodi.

“Tumeendelea kuthibitisha haya kwa vitendo kwa kushirikiana na Serikali kuboresha huduma za kijamii ikiwemo elimu, afya, maji, miundombinu yabarabara pamoja na shughuli mbalimbali za kuwawezesha wananchi kiuchumi maeneo yanayozungukamgodi,” alisema Jordinson.

Alisema mpango huo unaotumia bajeti ya Sh.1.3 bilioni za Kitanzania, unawalenga wajasiriamali 500 wanaoishi mkoani Geita wakiwemo vijana wanawake na watu wenye ulemavu.

“Kufuatia mabadiliko ya Sheria ya Madini ya mwaka2017, GGML kupitia fedha za Uwajibikaji wa Kampuni kwa Jamii imeshirikiana vyema na halmashauri mkoani Geita kutekeleza miradi ya maendeleo kwa jamii yenye thamaniya jumla ya shilingi za kitanzania bilioni 30 mkoani Geita,” alisema Jordinson.

Kwa upande wake, Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC), Beng’i Issa aliipongeza GGML kwa mpangohuo ambao unaendana na mpango wa kuendeleza biashara mkoani humo.

“Mpango huu utawajengea uwezo na kujiamini wajasiriamalina kushindana vyema na wafanyabiashara wengine nchini ili baadaye waweze kuboreshamapato na maisha yao,” alisema Beng’i Issa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Bodaboda waeleza mafanikio mafunzo usalama barabarani

Spread the loveMADEREVA bodaboda katika Jiji la Dodoma wameeleza jinsi mafunzo ya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yaahidi kuendelea kuunga mkono Serikali za Mitaa

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imesisitiza dhamira yake ya...

Habari Mchanganyiko

Watuhumiwa 12 wa kilo 726.2 za dawa za kulevya wafikishwa mahakamani

Spread the love  WATUHUMIWA watatu wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kibaha Mkoani...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

error: Content is protected !!