February 26, 2021

Uhuru hauna Mipaka

NECTA yatangaza matokeo ya kidato cha nne 2018

Dk. Charles Msonde, Katibu Mtendani wa NECTA

Spread the love

MATOKEO ya mtihani wa kidato cha nne ya watahiniwa wa shule yanaonesha kuwa idadi ya watahiniwa waliofaulu imeongezeka kwa asilimia 1.29 kutoka asilimia 77.09 ya mwaka 2017 hadi asilimia 78.38 mwaka 2018. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Aidha takwimu zinaonesha idadi ya watahiniwa waliopata ufaulu mzuri wa daraja I-III imeongezeka kwa mwaka 2018 na kuwa asilimia 31.76,ambapo mwaka 2016 ilikuwa ni asilimia 27.60 na mwaka 2017 ilikuwa 30.15.

Akizungumza jana Jijini hapa na Waandishi wa Habari, Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA) Dk. Charles Msonde alisema watahiniwa 322,965 sawa na asilimia 78.38 waliofanya mtihani wa kidato cha nne mwaka 2018 wamefaulu.

Alisema  wasichana walikuwa ni 163,820 sawa na asilimia 77.58 na wavulana ni 159,045 sawa na asilimia 79.23.

Katibu huyo Mtendaji alisema jumla ya watahiniwa 322,965 sawa na asilimia 78.38 waliofanya mtihani wa kidato cha nne mwaka 2018 wamefaulu huku wasichana wakiwa ni 163,820 sawa na asilimia 77.58 na wavulana ni 159,045 sawa na asilimia 79.23.

Dk Msonde alisema mwaka 2017 watahiniwa waliofaulu walikuwa ni 287,713 sawa na asilimia 77.09 ambapo ufaulu umeongezeka kwa asilimia 1.29 ikilinganishwa na mwaka 2017.

“Watahiniwa wa shule waliofaulu ni 284,126 sawa na asilimia 79.27 ya waliofanya mtihani ambapo wasichana waliofaulu ni 142,888 sawa na asilimia 78.51 na wavulana ni 141,238 sawa na asilimia 80.05.

“Mwaka 2017 watahiniwa 245,274 sawa na asilimia 77.57 ya watahiniwa wa shule walifanya mtihani huo hivyo ufaulu watahiniwa umeongezeka kwa asilimia 1.70 ikilinganishwa na mwaka 2017, alisema Dk. Msonde.

Alisema watahiniwa kujitegemea waliofaulu mtihani ni 38,839 sawa na asilimia 72.44 huku mwaka 2017 watahiniwa wa kujitegemea 42,439 sawa na 74.41 waliofanya mtihani huo,hivyo ufaulu umeshuka kwa asilimia 1.97 ikilinganishwa na mwaka 2017.

Kuhusiana na mtihani wa Maarifa (QT) waliofaulu ni 7,642 sawa na asilimia 62.46 ambapo mwaka 2017 watahiniwa wa mtihani wa maarifa 8,280 sawa na asilimia 60.11 walifaulu mtihani huo hivyo ufaulu umeongezeka kwa asilimia 2.35 ikilinganishwa na mwaka 2017.

Ubora wa ufaulu 

Dk. Msonde alisema ubora wa ufaulu unaonesha kuwa jumla ya watahiniwa waliopata ufaulu mzuri  wa madaraja ya 1-III ni 113,825 sawa na asilimia 31.76 wakiwemo wasichana 47,779 sawa na asilimia 26-25 na wavulana 66,046 sawa na asilimia 37-43.

Alisema mwaka 2017 idadi ya watahiniwa waliopata ufaulu wa madaraja I-III walikuwa 95,337 sawa na asilimia 30.15, hivyo ubora wa ufaulu umeongezeka kwa asilimia 1.61.

Ufaulu wa masomo kwa watahiniwa 

Dk. Msonde alisema ufaulu wa shule katika masomo ya Historia, Kiswahili, Physics, Chemistry, Basic Mathematic na Book-Keeping umepanda kati ya asilimia 0.83 na 8.76 ikilinganishwa na mwaka 2017.

Alisema ufaulu wa juu kabisa ni ule wa somo la Kiswahili ambapo asilimia 89.32 ya watahiniwa wote wa shule waliofanya somo hilo wamefaulu.

Alisema ufaulu wa chini kabisa ni ule wa somo la Basic Mathematics ambapo asilimia 20.02 ya watahiniwa wote wa shuler waliofanya somo hilo wamefaulu.

Shule zilizofanya vizuri 

Dk. Msonde alizitaja shule 10 zilizofanya vizuri katika mtihani huo na kwamba  shule ya St. Francis Girls ya Mbeya imeongoza katika matokeo hayo ikifuatiwa na Kemebos ya Mkoani Kagera.

Alizitaja shule zingine kuwa ni Marian Boys ya Mkoani Pwani,Ahmes ya Mkoani Pwani,Canossa ya Dar es salaam,Maua Seminary ya Kilimanjaro,Precious Blood ya Arusha,Marian Girls ya Pwani,Bright Future Girls ya Dar es salaam na Bethel Sabs Girls ya Iringa.

Aidha Dk. Msonde aliwataja watahiniwa 10  waliofanya vizuri katika mtihani huo ambapo Hope Mwaibaje wa Shule ya Ilboru ya mkoani Arusha ameongoza.

Aliwataja wengine na nafasi katika mabano kuwa ni Avith Kibani (2) kutokea shule ya Marian Boys ya Mkoani Pwani, Maria Manyama (3) kutokea shule ya St. Francis Girls ya Mbeya, Atughulile Mlimba (4) St. Francis Girls ya Mbeya.

Wengine ni Flavia Nkongoki (5) kutoka St. Francis Girls ya Mbeya, Leticia Ulaya (6) kutoka St. Francis Girls ya Mbeya, Gibson Katuma (7) Marian Boys ya Pwani, Bryson Jandwa (8) ya Pwani, Idegalda Kiluba (9) kutoka St. Francis ya mkoani Mbeya na Isack Julius (10) kutoka shule ya Marian Boys ya mkoani Pwani.

Aidha aliwataja wasichana 10 waliofanya vizuri katika matokeo hayo ambapo shule ya St. Francis Girls  imetoa wanafunzi 9 kati ya 10.

Dk. Msonde alisema  Maria Manyama, ameongoza katika matokeo hayo akifuatiwa na Atughulile Mlimba kutoka shule hiyo hiyo.

Aliwataja wengine ni Flavia Nkongoki (3), Letcia Ulaya (4), Idegalda Kiluba (5), Subilaga Mwaisela (6), Joyce Sapali (7), Ivony Anangisye (8), Saraha Kasala (9) St. Francis Girls na Theresia Karugwa (10) kutoka Anwarite Girls ya mkoani Kilimanjaro.

Kwa upande wa wanaume Hope Mwaibinje wa shule ya Ilboru ameongoza akifuatiwa na Avith Kibani wa shule ya Marian Boys ya Pwani.

Wengine ni Gibron Katuma (3) kutoka shule ya Marian Boys, Brison Jandwa (4) kutoka Marian Boys, Isack Julius (5) kutoka Marian Boys, Justine Byarasobile 6) kutoka Katoke Seminary ya Kagera.

Aliwataja wengine ni Emanuel Kandege (7) kutoka Uwata Mbeya, Saitoti Upendo (8) kutoka Ilboru ya Arusha, Peter Kiama kutoka Feza Boys ya Dar es salaam na David Sichone kutoka Pandahill ya Mbeya.

Katibu huyo Mtendaji alizitaja shule 10 za mwisho kuwa ni Pwani Mchangani (1) ya Kaskazini Unguja,Ukuta (2) ya Kusini Pemba, Kwediboma (3) ya Tanga, Rwemondo (4) ya Kagera, Namatula (5) ya mkoani Lindi.

Dk. Msonde alizitaja shule zingine kuwa ni Kijini (6) ya Kaskazini Unguja, Komkalakala (7) ya Mkoani Tanga, Kwizu (8) ya Mkoani Kilimanjaro, Seute (9) ya Mkoani Tanga na Masjid Qubah Muslim (10) ya Jijini Dar es salaam.

KUTAZAMA MATOKEO YOTE INGIA HAPA.

error: Content is protected !!