Saturday , 25 March 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko NECTA yapiga ‘stop’ kutangaza shule, watahiwani 10 bora
Habari Mchanganyiko

NECTA yapiga ‘stop’ kutangaza shule, watahiwani 10 bora

Kaimu Katibu Mtendaji wa Necta, Athumani Amasi
Spread the love

BARAZA la Mitihani la Taifa (NECTA) limetangaza kuondoa utaratibu wa kutangaza shule 10 bora na watahiniwa 10 bora kwa matokeo ya mitihani mbalimbali kwa kuwa utaratibu huo hauna tija. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 29 Januari 2023 jijini Dar es Salaam, Kaimu Katibu Mtendaji wa NECTA, Athuman Amas, amesema wameondoa utaratibu wa kutangaza shule 10 bora na watahiniwa 10 bora kwa sababu hauna tija.

“Tulizoea kusikia shule bora, mtahiniwa bora, wasichana wawagaragaza wanaume, tulizoea kwa muda mrefu kusikia hayo… sasa tuondokane na mazoea.

“Ukigundua jambo unalolifanya halina tija hauna haja ya kuendelea nalo, unamtaja mtu ameongoza na kumlinganisha na watu ambao hawakusoma katika mazingira yaliyofanana sio sahihi,” amesema.

Amesema kama kuna shule ilikuwa inasubiri itangazwe kuwa kwenye ‘Top 10’ hiyo haipo kwa sababu huwezi kutangaza shule moja wakati shule zipo zaidi ya 11,000.

“Kwanza kutangaza shule ya kwanza huenda tulikuwa tunakufanyia marketing (kukutangaza kibiashara), tumeona haina tija” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Watendaji Kata, Mitaa watakaoshindwa kusimamia usafi kukiona

Spread the love  WATENDAJI wa kata, mitaa na vitongoji na maofisa afya...

Habari Mchanganyiko

Mtia nia urais TLS kukata rufaa kupinga kuenguliwa

Spread the love  MTIA nia ya kugombea Urais wa Chama cha Mawakili...

Habari Mchanganyiko

NBC yazindua kampeni ya mkeka wa ushindi na ATM zake

Spread the loveBENKI ya Taifa ya Biashara (NBC) imetangaza uzinduzi wa kampeni...

Habari Mchanganyiko

Uholanzi wampongeza Rais Samia kuimarisha vyombo vya habari, demokrasia

Spread the love  UBALOZI wa Uholanzi nchini Tanzania, umempongeza Rais Samia Suluhu...

error: Content is protected !!