August 10, 2022

Uhuru hauna Mipaka

NECTA yajivunia mafanikio

Spread the love

BARAZA la Mitihani la Tanzania (NECTA) limejigamba kufanikiwa kudhibiti wizi wa mitihani ya Taifa na ngazi mbalimbali za elimu nchini, anaandika Aisha Amran.

Na kwamba, mafanikio hayo ni zao la ushirikiano kati ya NECTA na kamati za uendeshaji mitihani katika ngazi za mikoa na wilaya.

Hayo  yamebainishwa jana na Daniel Mafie Mkuu wa Idara ya Fedha na Utawala wa Baraza hilo  wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam uliolenga kueleza mafanikio yaliyofikiwa hadi sasa.

Amesema, katika mtihani wa kumaliza Elimu ya Msingi mwaka 2013, watahimiwa waliofutiwa matokeo kwa kufanya udanganyifu walikuwa 13 tu ikilinganishwa na watahiniwa 9,736 waliobainika kufanya udanganyifu mwaka 2011.

Mafie amesema, katika Mtihani wa Kidato cha Nne mwaka 2013 watahimiwa waliofutiwa matokeo kwa kufanya udanganyifu walikuwa 272 ikilinganishwa na watahimiwa 789 mwaka 2012 na 3,303 mwaka 2011.

Akieleza zaidi kuhusu mafanikio yaliyofikiwa amesema, baraza hilo limeweza kusanifu mifumo ya Kompyuta yenye uwezo wa kupanga shule katika makundi ya ubora wa ufaulu katika matokeo ya mitihani ya Taifa.

Katika kukabiliana na tatizo la watu wanaotumia vyeti vya watu wengine au kughushi vyeti wakati wa kuomba ajira au nafasi za masomo katika shule mbalimbali ambapo kuanzia mwaka 2008/2009 baraza hilo lilianzisha utaratibu wa kuweka picha za watahimiwa katika vyeti vyao.

Amesema katika utaratibu huo vyeti hivyo viliwekewa alama za kiusalama hali ambayo imesaidia Baraza hilo kuwa na uwezo wa kubaini kwa haraka na kuwachukulia hatua wale wanaoghushi vyeti au kutumia vyeti vya watu wengine.

 

error: Content is protected !!