Tuesday , 30 May 2023
Home Gazeti Habari za Siasa NEC yapigwa ‘stop’ kufanya haya
Habari za SiasaTangulizi

NEC yapigwa ‘stop’ kufanya haya

Spread the love

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) nchini Tanzania haipaswi kufanya mambo makuu manne wakati wa mchakato wa Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Mambo hayo ni miongoni mwa Maadili ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya mwaka 2020.

Mambo hayo ambayo NEC haipaswi kufanywa ni; kupendelea chama chochote cha siasa au mgombea yeyote. Kubadili ratiba za kampeni za uchaguzi bila kushirikisha vyama vya siasa.

Pia, NEC haipaswa kuchelewa au kupeleka vifaa pungufu katika vituo vya kupigia kura bila sababu za msingi na mwisho kuchelewa kutangaza matokeo ya uchaguzi bila sababu za msingi.

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Dk. Wilson Mahera

Katika maadili hayo, miongoni mwa mambo yanayotakiwa kufanywa na NEC ni kupanga, kusimamia na kuendesha uchaguzi katika misingi inayowezesha uchaguzi kuwa huru na wa haki.

Kuzingatia Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, sharia za uchaguzi na sharia nyingine za nchi;kuvipatia vyama vya siasa ratiba na taarifa za uchaguzi kwa wakati na kuratibu matumizi ya vyombo vya habari vya umma ili kutoa fursa sawa kwa wagombea urais na makamu wa Rais na vyama vyao.

NEC inaratibu kamati za kusimamia maadili ya uchaguzi pamoja na kusimamia utekelezaji wa maamuzi yanayotolewa na kamati hizo na kuandaa na kupeleka kwa wakati vifaa vya kutosha kwenye vituo vya kupigia kura.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Uamuzi juu ya wakurugenzi kusimamia uchaguzi 13 Juni

Spread the love  MAHAKAMA ya Afrika ya Haki za Binadamu (ACHPR), imepanga...

Habari MchanganyikoTangulizi

Jeshi la Polisi kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika utafiti

Spread the love  JESHI la Polisi Nchini limesema kuwa katika kukabiliana na...

KimataifaTangulizi

Mtuhumiwa wa mauaji ya halaiki ya Rwanda akamatwa Afrika Kusini

Spread the love  MMOJA wa watuhumiwa wakuu wa mauaji ya Kimbari ya...

Habari za Siasa

Musoma Vijijini waomba ujenzi wa barabara uanze haraka

Spread the loveJIMBO la Musoma Vijijini, mkoani Mara, limeomba Serikali kuhakikisha ujenzi...

error: Content is protected !!