Tuesday , 5 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa NEC yawanoa wasimamizi wa uchaguzi, yawapa onyo
Habari za Siasa

NEC yawanoa wasimamizi wa uchaguzi, yawapa onyo

Wasimamizi wa uchaguzi wakila kiapo cha kusimamia Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020
Spread the love

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imewataka wasimamizi wa Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Jumatano tarehe 28 Oktoba 2020 kuzingatia weledi na kuepuka kufanya kazi kwa mazoea ili kupunguza au kuondoa kabisa malalamiko yanayoweza kujitokeza wakati wa uchaguzi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma …(endelea).

Hayo yamesemwa leo Jumatatu tarehe 27 Julai 2020 na Mjumbe wa NEC, Balozi Omari Ramadhani Mapuri wakati akifungua mafunzo ya siku tatu jijini Dodoma yaliyokutanisha washiriki 162 ambao ni wasimamizi wa uchaguzi kanda ya kati.

Balozi Mapuri amewataka kuzingatia maadili wanapofanya kazi hiyo kwani uchaguzi ni mchakato unaojumuisha hatua na taratibu mbalimbali zinazopaswa kufuatwa na kuzingatiwa.

Mjumbe wa NEC, Balozi Omari Ramadhani Mapuri wakati akifungua mafunzo ya siku tatu jijini Dodoma

Amesisitiza hatua na taratibu hizo ndiyo msingi wa uchaguzi mzuri wenye ufanisi usio na malalamiko.

Balozi Mapuri amesema, wasimamizi hao, katika mkutano huo wa siku tatu wanatakiwa kubadilishana uzoefu, kujadili namna bora ya kufanikisha uchaguzi, lakini pia kujadili namna bora ya kukabiliana na changamoto zinazoweza kujitokeza katika hatua mbalimbali za uchaguzi.

Aidha Balozi Mapuri, amewataka wasimamizi hao kufanya kazi kwa kufuata maadili kwa kuzingatia sheria, kanuni pamoja na maagizo na maelekezo yanayotolewa na NEC.

“Mnatakiwa kutumia mkutano huu, kubadilisha uzoefu na kufanya kazi kwa kufuata maadili kwa kuzingatia sheria, kanuni na maelekezo pamoja na maagizo ya Tume ya uchaguzi,” amesema.

Wasimamizi wa uchaguzi wakisikiliza kwa makini kinachoendelea katika semina hiyo

Balozi Mapuri amesema, wasimamizi hao wameaminiwa na kuteuliwa na tume katika nafasi hizo za usimamizi wa uchaguzi kwa kuwa wana uwezo wa kufanya kazi hiyo hivyo wanatakiwa wajiamini na kujitambua.

Ametoa mwito kwa wasimamizi hao kuhakikisha wanayaelewa vema maeneo yao ya kazi kijiografia na kuhakikisha wanawatumia vizuri wasaidizi walio chini yao katika maeneo yao ili kutoa matokeo bora.

Pia, amewataka wasimamizi hao kujua miundombinu mbalimbali ya kufika kwenye vituo vya kupigia kura katika majimbo wanayosimamia uchaguzi.

Balozi Mapuri amewataka washirikishane na vyama vya siasa pamoja na wadau wengine wa uchaguzi katika mstakabali mzima wa uchaguzi ili kuongeza uwazi katika uchaguzi na hivyo kuleta ufanisi.

Wasimamizi wa uchaguzi

Kati ya washiriki wa mkutano huo, wasimamizi wa uchaguzi wapo 24, wasimamizi wasaidizi uchaguzi katika majimbo wapo 87, maafisa uchaguzi 24, waratibu wa uchaguzi watatu na maafisa ugavi 24 ambapo kati yao 55 wanatoka mkoa wa Dodoma, Morogoro 61 na Singida 46.

Katika kwenda kutekeleza kikamilifu majukumu yao usimamizi hao katika uchaguzi huo wamekula viapo viwili moja cha kujitoa katika vyama vya siasa na nyingine ya kutunza siri za uchaguzi wanaposimamia uchaguzi.

Kiapo hicho cha utii kiliongozwa na Hakimu Mkazi Mfawidhi Mwandamizi Wilaya ya Dodoma, Mary Senapee ambaye aliwataka washirikishi hao kusaini baada ya kuapa kwani wakikiuka maadili ya uchaguzi ndicho kitakacho wafunga.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Dk. Biteko: Viongozi tuache alama nzuri katika utendaji wetu

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za SiasaTangulizi

Chanzo maporomoko yaliyoua 65 Hanang, chatajwa

Spread the loveSERIKALI imesema kumeguka kwa sehemu ya Mlima Hanang ambao ilikuwa...

Habari za Siasa

Baba yake Ole Sabaya ashinda Uenyekiti CCM – Arusha

Spread the loveLoy Thomas Sabaya ambaye ni Baba wa aliyekuwa Mkuu wa...

Habari za Siasa

Serikali yaagiza uchunguzi chanzo maporomoko Hanang

Spread the loveSERIKALI imeagiza uchunguzi ufanyike ili kubaini chanzo cha maporomoko ya...

error: Content is protected !!