Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa NEC yaunda kamati kuchunguza pingamizi, malalamiko
Habari za Siasa

NEC yaunda kamati kuchunguza pingamizi, malalamiko

Mwenyekiti wa NEC, Semistocles Kaijage
Spread the love

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imeunda Kamati za Maadili ili kushughulikia pingamizi na malalamiko ya wagombea kuhusu ukiukwaji wa maadili ya uchaguzi mkuu wa tarehe 28 Oktoba 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

 Taarifa hiyo imetolewa na Jaji Semistocles Kaijage, Mwenyekiti wa NEC ambapo amesema, kamati hizo zitakazoanzia ngazi ya kata, ubunge hadi Taifa, zitahusisha wajumbe kutoka kila chama kilichosimamisha mgombea katika ngazi husika.

Jaji Kaijage amesema, kamati hizo zimepewa uwezo wa kuyashughulikia malalamiko ya ukiukwaji wa maadili ya uchaguzi, na kwamba kama mlalamikaji asiporidhika na uamuzi wake katika ngazi husika, anaweza kukata rufaa.

“Kamati za maadili tayari zimeundwa kuanzia ngazi ya kata kwa uchaguzi wa madiwani, ngazi ya jimbo kwa uchaguzi wa wabunge na gazi ya taifa kwa ajili ya uchaguzi wa rais na makamu wa rais, ile vile kuna kamati ya rufaa kwa wale ambao hawataridhika na maamuzi ya kamati nyingine,” amesema Jaji Kaijage na kuongeza:

 “Katika uchaguzi wa mwaka huu, tume haitarajii kuona vyamavya siasa vikilalamika kuhusu ukiukwaji wa maadili ya uchaguzi,  badala yake kuchukua hatua stahiki za kisheria kwenye mamlaka husika.

Dk. Wilson Mahera, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC

“Hatua hizo ni pamoja na kuzitumia kamati za maaidli ambazo zimepewa mamlaka kushughiulikia malalamiko yanayohusu ukiukwaji wa maadili ya uchaguzi hususan katika kipindi cha kampeni.”

Wakati huo huo, Jaji Kaijage amesema, NEC imepokea rufaa 557 kutoka kwa wagombea wa ubunge na udiwani, ambao hawajaridhika na uamuzi wa wasimamizi wa uchaguzi.

 “Hivi sasa tume ipo katika hatua ya kupokea rufaa kutoka majimboni kwa ajili ya wagombea ubunge na kutoka katika kata mbalimbali kwa ajili ya wagombea udiwani, rufaa hizi zinatokana na baadhi ya wagomea ubunge na udiwani kutoridhika na maamuzi ya wasimamizi wa uchaguzi,” amesema Jaji Kaijage.

Mwenyekiti huyo wa NEC amesema, tume hiyo imeanza kuzifanyia kazi rufaa hizo kuanzia jana na kwamba itazitolea uamuzi mapema iwezekanavyo.

“Hadi hivi sasa tume imepokea jumla ya rufaa 557 ambazo itaanza kuzifanyia kazi leo (jana)na itajitahidi kuzitolea uamuzi mapema kwa kadri itakavyowezekana,” ameahidi Jaji Kaijage.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Tanzania, Uturuki zanuia kukuza biashara, uwekezaji

Spread the loveSERIKALI za Tanzania na Uturuki zimekubaliana kuendeleza dhamira ya kuimarisha...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

Habari za Siasa

CCM yamkana mwenyekiti UVCCM aliyetaka wapinzani wapotezwe

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimejitenga na kauli ya mwenyekiti...

error: Content is protected !!