Sunday , 25 February 2024
Home Gazeti Habari za Siasa NEC yateua madiwani 12 viti maalum
Habari za Siasa

NEC yateua madiwani 12 viti maalum

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchuguzi (NEC), Ramadhani Kailima
Spread the love

Tume ya Taifa ya uchaguzi Tanzania (NEC) imeteua madiwani 12 wa viti maalum kujaza nafasi zilizokuwa wazi katika halmashauri mbalimbali Tanzania Bara, anaandika Hamisi Mguta.

Taarifa iliyowekwa na Mkurugenzi wa Tume hiyo, Ramadhan Kairima katika tovuti ya Tume imeeleza kuwa uteuzi huo ni kwa Mujibu wa Kifungu cha 86A (8) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) katika kikao chake cha kawaida kilichofanyika leo tarehe 21 Agosti, 2017 na baada ya kushauriana na Vyama vya Siasa.

Madiwani Wanawake wa Viti Maalumu walioteuliwa ni kama ifuatavyo:

 

NA. JINA CHAMA HALMASHAURI
      1 Ndugu Saida Idrisa Kiliula CUF Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa
     2 Ndugu Sophia Charokiwa Msangi CCM Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga
    3 Ndugu Shahara Selemani Nduvaruva CCM Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali
    4 Ndugu Neema K. Nyangalilo CCM Halmashauri ya Manispaa ya Ilala
    5 Ndugu Farida Zaharani Mohamed CCM Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero
    6 Ndugu Lucia Silanda Kadimu CCM Halmashauri ya Wilaya ya Tabora (Uyui)
    7 Ndugu Amina Ramshi Mbaira CCM Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu
     8 Ndugu Janeth John Kaaya CHADEMA Halmashauri ya Wilaya ya Meru
      9 Ndugu Sara Abdallah Katanga CHADEMA Halmashauri ya Manispaa ya Ilala
      10 Ndugu Ikunda Massawe CHADEMA Halmashauri ya Wilaya ya Hai
       11 Ndugu Tumaini Wilson Masaki CHADEMA Halmashauri ya Wilaya ya Siha
       12 Ndugu Elizaberth Andrea Bayyo CHADEMA Halmashauri ya Mji wa Mbulu

Uteuzi huu umefanyika baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Waziri mwenye dhamana ya Serikali za Mitaa ambaye kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 13(1) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292 alitaarifu Tume ya Taifa ya Uchaguzi uwepo wa nafasi hizo wazi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Samia atoa pole ajali iliyoua 25, kujeruhi 21 Arusha

Spread the loveRais Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za rambirambi kwa Mkuu...

Habari za SiasaTangulizi

Dk. Biteko afuta likizo watumishi Tanesco, bosi Morogoro yamkuta

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dk. Doto...

Habari za Siasa

Mbarala ajitosa kumrithi Zitto, aahidi kuipa ushindi ACT-Wazalendo uchaguzi mkuu

Spread the loveKATIBU wa Idara ya Haki za Binadamu na Makundi Maalum...

Habari za Siasa

Dorothy Semu ajitosa kumrithi Zitto ACT-Wazalendo

Spread the loveMAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha ACT-Wazalendo, anayemaliza muda wake, Dorothy...

error: Content is protected !!