Monday , 30 January 2023
Home Gazeti Habari za Siasa NEC yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Ngorongoro
Habari za Siasa

NEC yatangaza uchaguzi mdogo Jimbo la Ngorongoro

Mkurugenzi wa Uchaguzi, Dk. Wilson Mahera
Spread the love

 

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imetangaza uchaguzi mdogo katika Jimbo la Ngorongoro, mkoani Arusha na Kata ya Naumbu mkoani Mtwara, ili kujaza nafasi zilizoachwa wazi katika maeneo hayo kufuatia viongozi wake kufariki dunia. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Taarifa hiyo imetolewa leo Jumatatu, tarehe 18 Oktoba 2021 na Mkurugenzi wa Uchaguzi NEC, Dk. Wilson Mahera.

Kwa mujibu wa taarifa ya Dk. Mahera, zoezi la uchukuaji fomu za uteuzi kugombea nafasi hizo litafanyika kuanzia tarehe 7 hadi 15 Novemba 2021 ambayo pia itakuwa siku ya uteuzi wa wagombea, huku kampeni za uchaguzi zikianza tarehe 16 Novemba hadi 10 Disemba mwaka huu.

Uchaguzi huo mdogo unatarajiwa kufanyika tarehe 11 Disemba 2021.

Taarifa ya Mahera imesema, imeitisha uchaguzi mdogo wa Jimbo la Ngorongoro, baada ya kupokea barua kutoka kwa Spika wa Bunge, iliyitaarifu kuwepo kwa nafasi wazi ya ubunge, iliyotokana na kufariki kwa aliyekuwa Mbunge wake, William Tate Ole Nasha.

“Nafasi ya Jimbo la Ngorongoro ilitokana na kufariki kwa aliyekuwa mbunge wake, kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), tarehe 27 Septemba 2021. Mheshimiwa ametoa taarifa hiyo kwa mujibu wa kifungu cha 37 (3) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343,” imesema taarifa ya Dk. Mahera.

Taarifa ya Dk. Mahera imesema, uchaguzi mdogo wa Kata ya Naumbu umeitishwa kufuatia kifo cha aliyekuwa diwani wake, kupitia Chama cha Wananchi (CUF), Rashid Julius Aderehemani, kilichotokea tarehe 29 Agosti mwaka huu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Chongolo asikitishwa na mradi wa Mil 900 kutoanza kutoa manufaa

Spread the loveKATIBU mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Daniel Chongolo...

Habari za Siasa

NCCR-mageuzi yawaangukia Polisi kupotea kwa kada wake

Spread the loveJESHI la Polisi nchini limeombwa kufanya uchunguzi wa kina utakaosaidia...

Habari za Siasa

Uamuzi kesi ya kupinga Bodi ya Wadhamini NCCR-Mageuzi kutolewa Februari 6

Spread the love  MAHAKAMA Kuu, Masjala Kuu ya Dar es Salaam, imepanga...

Habari za SiasaTangulizi

Lissu:Suluhu ya ugumu wa maisha ni Katiba Mpya

Spread the love  MAKAMU mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo-Chadema Bara,...

error: Content is protected !!