July 7, 2022

Uhuru hauna Mipaka

NEC yapigwa jeki

Mkurugenzi wa Kampuni ya Masoko, Conctantine Magavila (katikati) akizungumza na waandishi wa habari. Kulia ni mwanamuziki Snura Mushi, kushoto Afisa Elimu wa NEC, Rose Mongi.

Spread the love

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imesema haina fedha za kutosha kuendesha kampeni mbalimbali za kuhamasisha wananchi kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura, hivyo inategemea makampuni mbalimbali kujitolea. Anaandika Sarafina Lidwino … (endelea).

Afisa Elimu wa NEC kitaifa, Rose Mongi ndiye alitoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam, wakati akizindua kampeni maalumu ya kuhamasisha vijana kujitokeza katika uandikishaji na siku ya kupiga kura.

Mongi amesema, makampuni yoyote yenye uwezo wa kuendesha kampeni yoyote yenye kutoa elimu juu ya upigaji kura waandelee kuisaidia NEC haswa kwa kipindi hiki kigumu.

Kampeni hiyo imeandaliwa na Kampuni ya Masoko inayojihusisha na masuala ya mawasiliano na masoko, Shirika la Openi Society International East Afrika (OSIEA) na NEC, wakiwa na lengo la kuhakikisha vijana wanashiriki kujiandikisha.

Naye Mkurugenzi wa Masoko, Constantine Magavila amesema, wameamua kuanzisha kampeni hizo ili kuweza kuwafikia watu wengi zaidi mijini na vijijini.

“Tumegundua kuwa, vijana wanaweza kuleta mabadiliko makubwa endapo watajitokeza kupiga kura kwa wingi,“ amesema Magavila.

Ameongeza kuwa, kampeni hiyo inatarajia kuhusisha mikoa mitano ikiwemo Dar es Salaam, Morogoro, Mwanza, Geita na Shinyanga, ambapo yatafanyika matamasha mbalimbali ambayo hayana viingilio.

“Tumefanya mikoa hiyo mitano lakini tunaamini kwa kushirikiana na vyomba vya habari ujumbe utafika nchi nzima,”amesema.

Kwa mujibu wa Magavila, wasanii watano wametunga wimbo maalumu wa kuhamasisha uitwao “Kura Dili”, ambao wanaamimini utawaamsha vijana wengi ili kuweza kutambua umuhimu wao.

“Tunaamini kampeni hii itakuwa na mafanikio makubwa na uchaguzi wa mwaka huu utavunja rekodi kwa vijana wote kushiriki katika upigaji kura.”

error: Content is protected !!