July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

NEC yaonya wanasiasa

Mwenyekiti Tume ya Uchaguzi, Jaji Damian Lubuva

Spread the love

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imewaonya wanasiasa wanaoingilia zoezi la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kupitia mfumo wa mashine za kielektroniki (BVR) na kusababisha vurugu katika baadhi ya maeneo. Anaandika Jimmy Mfuru … (endelea).

Na kwamba, sehemu zote ambako zoezi hilo limepita Arusha ndio imeonesha kuwa kinara wa  vurugu ukilinganisha na mikoa mingine zoezi hilo lilikopitia.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Damian Lubuva, alipokuwa akielezea hali ya uandikishaji inavyoendelea na vurugu zilizotokea Arusha.

“Kati ya sehemu zote ambazo zoezi hili limepitia Arusha ndio imeonekana kinara wa vurugu kwa baadhi ya wanasiasa kufanya uchochezi,”amesema Jaji Lubuva na kuongeza;

Wanasiasa hao hasa wa chama cha Chadema wametakiwa kuiacha tume kufanya kazi yake badala ya kuingilia na kusababisha vurugu ambazo hazina tija.

Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Godbless Lema aliswekwa mahabusu kwa saa 2 baada ya polisi kumkamata kwa madai ya kufanya vurugu katika kituo cha uandikishaji.

Polisi walimkamata mbunge huyo juzi usiku na kumuweka mahabusu usiku akiwa na wafuasi wake.

Lema alikuwa kwenye Kata ya Olsunyai Manispaa ya Arusha, akizungukia waandikishwaji wa daftari la wapigakura kwa kutumia mfumo wa BVR ili kujionea hali halisi ilivyo.

Lema alitiwa mbaroni kwa tuhuma za kuchochea vurugu kituoni hapo.

error: Content is protected !!