January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

NEC yaongeza uandikishaji BVR Dar

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, Damian Lubuva

Spread the love

TUME ya Taifa ya uchaguzi (NEC) leo imeongeza siku nne za kuendelea na zoezi la uandikishaji katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kupitia mfumo wa Kielektroniki (BVR), baada ya kuona muda hautoshi Jijini Dar es Salaam. Anaandika Sarafina Lidwino … (endelea).

Hatua hiyo imekuja baada ya zoezi hilo kuonekana kukwama katika baadhi ya maeneo Jijini Dar es Salaam na kusababisha kutofikia malengo ya NEC mbapo walipanga kumaliza Julai 31 mwaka huu hivyo baada ya kuongeza siku hizo zoezi hilo sasa litamalizika agosti 04 mwaka huu ili kuwapa fursa zaidi wananchi kujiandikisha.

Taarifa hiyo ni kwa mujibu wa Mwenyekiti wa tume hiyo Jaji Damian Lubava katika taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari mapema leo.

Mabadiliko hayo yamekuja baada ya Lubuva kupokea malalamiko mengi kutoka kwa wananchi ya kwamba, wananchi wengi bado hawajapata fursa ya kujiandikisha na kwamba, muda uliopangwa hautoshi.

error: Content is protected !!