Sunday , 2 April 2023
Habari za Siasa

NEC yamuonya Lissu

Spread the love

KAMATI ya Maadili ya Kitaifa ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) nchini Tanzania imemuonya Tundu Lissu, mgombea urais kupitia Chadema kutekeleza adhabu aliyopewa ya kutofanya kampeni siku saba kuanzia leo hadi 9 Oktoba 2020. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Jana Ijumaa tarehe 2 Oktoba 2020, kamati hiyo ilitangaza kumfungia kwa siku hizo baada ya kupokea malalamiko kutoka yaliyowasilishwa na vyama vya NRA na CCM vikimtuhumu Lissu kutoa maneno ya uchochezi yasiyothibitika.

Hata hivyo, Lissu alipinga adhabu hiyo kwa kile alichoeleza, hakupewa malalamiko hayo yeye mwenyewe kwa njia ya maandishi wala kusikilizwa utetezi wake hivyo kudai ataendelea na ratiba zake za kampeni kesho Jumapili Mkoa wa Pwani.

Lissu alisema, huo ni uamuzi wake binafsi na alikuwa anasubiri kamati kuu ya Chadema itaamua nini juu ya kilichofanywa na kamati hiyo kwenye kikao cha dharula kinachoendelea leo Jumamosi jijini Dar es Salaam.

Baada ya maelezo hayo, leo Jumamosi, Katibu wa Kamati hiyo ya maadili ya Kitaifa, Emmanuel Kawishe ametoa ufafanuzi wa uamuzi huo na madai ya Lissu kwamba amehukumiwa pasina kusikilizwa.

“Adhabu inatakiwa kutekelezwa kwa kuwa imetolewa na chombo chenye mamlaka ya kisheria na kwa kuzingatita taratibu. Mgombea wa kiti cha Rais kupitia Chadema anatakiwa kuheshimu na kutekeleza adhabuy hiyo kama ilivyotolewa,” amesema Kawishe

“Endapo mgombea huyo atadharau uamuzi wa kamati na kufanya kampeni atambue kuwa, kamati imepewa mamlaka ya kuelekeza makosa mengine kwenye vyombo vingine kadri itakavyoona inafaa kama ilivyoainishwa kwenye kanuni ya 5.7(1) ya Maadili ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani,” amesema Kawishe

Soma taarifa yote ya Kawishe hapa chini;

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia apangua mawaziri

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan, amefanya mabadiliko madogo ya Baraza la...

Habari za Siasa

RC mstaafu afariki dunia, CCM yamlilia

Spread the loveALIYEWAHI kuwa mkuu wa mikoa ya Dodoma, Mara, Mtwara na...

Habari za Siasa

Marekani kuwekeza Dola 500 Mil kupeleka bidhaa na huduma Tanzania

Spread the loveMAKAMU wa Rais wa Marekani, Kamala Harris amesema miongoni mwa...

Habari za Siasa

Kamala ataja hatua mpya kuimarisha uhusiano wa kibiashara Tanzania, Marekani

Spread the loveKATIKA kuimaridha uhusiano wa kibiashara na kiuchumi baina ya Tanzania...

error: Content is protected !!