August 13, 2022

Uhuru hauna Mipaka

NEC yaiongezea ‘power’ Chadema

Spread the love

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imekiongezea nguvu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa kukipa mbunge mmoja mpya, anaandika Wolfram Mwalongo.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya Jimbo la Kijitoupele visiwani Zanzibar kufanya uchaguzi wakati wa uchaguzi wa marudio uliofanyika tarehe 20 Machi mwaka huu hivyo kukamilisha mchakato wa uchaguzi katika majimbo yote bara na visiwani.

Kwenye jimbo hilo Shamsi Vuai Nahodha ameibuka mshindi, hata hivyo NEC imekipa Chama Cha Mapinduzi (CCM) viti viwili vya wabunge wa viti maalum.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Jaji Mstaafu, Damian Lubuva Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) amesema kuwa, uchaguzi umekamilika katika majimbo nane.

Uchaguzi huo ulihusu majimbo ya Tanzania Bara saba na Zanzibar moja ambalo ni Jimbo la Kijitoupele. Viti maalum vimetokana na kura za jumla za wabunge wote.

Walioteuliwa baada ya mchakato huo ni, Ritha Kabati (CCM), Oliver Semunguruka (CCM) pamoja na Lucy Owenya (Chadema).
Lubuva amesema kuwa, hatua hiyo imekamilisha uchaguzi kutokana na viti hivyo kupatikana na hivyo kufanya viti maalumu kuwa 113.

Katika mgawanyo wa viti hivyo CCM ina jumla ya viti 66,   Demokrasia viti 35 na Chama cha Wananchi (CUF) viti 10.

 

error: Content is protected !!