TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) nchini Tanzania, imemrejesha Jesca Kishoa kuwa mgombea ubunge Iramba Magharibi Mkoa wa Singida kupitia Chadema. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Jesca aliyekuwa mbunge wa viti maalum, atachuana na wagombea wa vyama vingine akiwemo Dk. Mwigulu Nchemba wa CCM.
Uamuzi uliotolewa jana Ijumaa tarehe 11 Septemba 2020 na Mkurugenzi wa Uchaguzi, Dk. Wilson Mahera ilisema tume hiyo ilizipitia, kuchambua na kuzifanyia uamuzi rufaa 60 kati ya hizo, mbili za wabunge na 58 za udiwani.
Soma zaidi:-
Dk. Mahera alisema, “imekubali rufaa moja na kumrejesha mgombea katika orodha ya wabunge. Rufaa hiyo ni kutoka jimbo la Iramba Magharibi.”
Ingawa taarifa hiyo ya Dk. Mahera kutomtaja jina la mgombea lakini Jecsa mwenyewe aliandika kwenye kwenye ukurasa wake wa Twitter akishukuru kwa uamuzi huo wa NEC.
“Nashukuru Mungu kwa hili, sasa kazi ni moja tu, kulikomboa jimbo la Iramba,” aliandika Jesca ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Baraza la Wanawake wa Chadema-Bara (Bawacha).

Katika uamuzi mwingine, Dk. Mahera alisema Tume imekataa rufaa moja ya mgombea ubunge wa Iramba Magharibi ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.
Dk. Mahera alisema, Tume ilizipitia, kuzichambua na kuzifanyia uamuzi rufaa 58 za madiwani kati ya hizo 34 imezikubali na kuwarejesha wagombea katika orodha ya wagombea udiwani huku ikizikataa rufaa 23 za wagombea.
Taarifa yote ya Dk. Mahera hii hapa chini;
Leave a comment