March 4, 2021

Uhuru hauna Mipaka

NEC wamrudisha rasmi Chiza Buyungu

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uwekezaji na Uwezeshaji), Mhandisi Christopher Chiza

Spread the love

MSIMAMIZI wa Uchaguzi Jimbo la Buyungu, Lusubilo Mwakabibi amemtangaza Christopher Chiza, Mgombea wa CCM kuwa mshindi wa uchaguzi mdogo wa jimbo hilo uliofanyika jana tarehe 12 Agosti, 2018. Anaripoti Regina Kelvin … (endelea).

Mwakabibi amemtangaza Chiza kuwa mshindi alfajiri ya leo tarehe 13 Agosti 2018.

Mwakabibi ametangaza kuwa, Chiza ameshinda kwa kura 24,578 huku aliyekuwa mpinzani wake wa karibu Eliah Michael wa Chadema akipata kura 16,910.

Jumla ya kura zilizopigwa na wakazi wa Buyungu zilikuwa 42,356 kati ya idadi ya watu 61,980 waliojiandikisha kupiga kura. Kati ya kura hizo, halali zilikuwa 41,841 na zilizoharibika ni 515.

error: Content is protected !!