January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

NEC waapa kula sahani moja na wabaya wa Lowassa

Spread the love

MWENYEKITI wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Damian Lubuva ametoa ovyo kali na kuahidi kuwachukulia hatua za kisheria, wanasiasa na wagombea wanaofanya kampeni chafu kwa kutaja majina ya watu, pamoja na kuingilia kazi za NEC. Anaandika Sarafina Lidwino … (endelea).

Anadai, amekuwa akishangwazwa sana na kitendo cha baadhi ya wagombea kupanda majukwaani kuwasema vibaya wagombea wenzao na kuwakashifu badala ya kutumia nafasi hiyo kwa kutangaza sera za chama na wagombea.

Hayo ameyasema leo Jijini Dar es Salaam katika hoteli ya New Afrika alipokutana na wawakilishi wa walemavu nchini ili kuzungumzia masuala mbalimbali ya uchaguzi likiwemo la kuwapo utaratibu wa kupiga kura.

Kabla ya utaratibu wa upigaji kura kwa walemavu kutolewa, Lubuva pia amevitaka vyama vya siasa kutokuwa na wasiwasi na NEC kama ilivyo kwa baadhi ya vyama ambavyo vinaonekana kutoiamini tume hiyo na kuwataka wanasiasa wanaona mwanya wa kuiba kura, wampe taarifa ili wazifanyie kazi.

“Kuna baadhi ya wanasiasa sitawataja lakini nawasikia wakiwasisitiza wanachama wao kutoondoka katika vituo vya kupigia kura siku hiyo kwa kigezo cha kulinda kura.

“Huo ni upotoshaji na ni kujisumbua, kwani hakuna kura itakayoibiwa kila mtu akimaliza arudi kwao na kusubiri matokeo,” amesema Lubuva.

Neye Kaimu Mkurugenzi wa NEC, Emmanuel Kawishe wakati akitoa maelekezo kwa walemavu hao amesema, siku hiyo ya uchaguzi, walemavu wote hawatakaa foleni bali watapita moja kwa moja sehemu ya kupigia kura.

Kawishe amesema kundi hilo na makundi maalumu likiwemo la wazee, wajawazito hawatakaa foleni pia. Na kwa wale walemavu wa macho wataruhusiwa kwenda na wasaidizi wao ndani ya chumba cha kupigia kura.

“Lakini tunawakumbusha tu makundi hayo ya walemavu wachague wasaidizi wasiohusika na uongozi katika chama chochote na wala asiwe wakala wa chama au Tume ili kuepusha ulaghai na wizi wa kura,” amesema Kawishe.

Pia amesema NEC inampango wa kuweka makaratasi maalumu ya kuandikia kwa wale wenye ulemavi wa macho pamoja kuandika maandishi makubwa ya wagombea ili kuwasaidia wenye matatizo ya kuona kama walemavu wa ngozi (Albino).

“Nadhani tutakuwa tumezingatia maombi yenu kwenye mchakato wa upigaji kura, tumeweka vituo katika maeneo rafiki kwenu na tumefanya hivyo, vituo vyote 72,000 vilipo katika maeneo mazuri mtakayoweza kwenda,” amesema Kawishe.

Amesema vituo vyote vitafunguliwa saa 1:00 asubuhi na kufugwa saa 12:00 ambapo mawakala wote wanatakiwa kuwepo katika chumba cha kupigia kura.

“Lakini kwa wakala ambaye hatakuwepo zoezi litaendelea kama kawaida hatutasitisha zoezi ili kumsubiri,” amesema Kawishe.

Aidha, Mkurugenzi huyo ametoa ufafanuzi juu ya Majimbo na Kata zote ambazo vyama vya siasa vimepoteza wagombea wao, Oktoba 12 hadi Novemba 22 vyama vinatakiwa kumteua mgombea mwingine ili kuziba pengo.

 

error: Content is protected !!