October 26, 2021

Uhuru hauna Mipaka

NEC, UNDP zazindua mawasiliano ya mpiga kura

Spread the love

IKIWA zimebaki siku 10 kufikia Uchaguzi Mkuu Oktoba 25 mwaka huu, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Kimataifa (UNDP) leo wamezindua kituo maalumu cha mawasiliano ili kuwawezesha Watanzania kuuliza maswali na kupata elimu ya mpiga kura. Anaandika Sarafina Lidwino … (endelea).

Akizungumza na waandishi baada ya kuzindua kutuo hicho, Mkurugenzi wa NEC, Ramadhani Kailima amesema kituo hicho kipo maalumu kwa ajili ya kupokea na kujibu maswali yote yanayohusu Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani.

Amesema kuanzia Oktoba 12 – 18 mwaka huu kituo kitafanya kazi kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa 12 jioni, na kuanzia Oktoba 19 -30 mwaka huu kituo hicho kitafanya kazi kwa saa 24.

Ramadhani amesema, kituo hicho kilianza kupokea simu tangu Oktoba 12 mwaka huu, ambapo jumla ya simu 444 zilipokelewa na jana zilipokewa simu 937.

Ameeleza kwamba kwa mwananchi yoyote akitaka kupata huduma hiyo anatakiwa kupiga simu kwa namba, 0800782100 na kuwa simu hiyo ni bure ambapo mtu ataweza kuuliza ama kutoa taarifa yoyote juu ya uchaguzi mkuu.

Aidha, wapokeaji simu na watoaji wa majibu yote ni watumishi wa NEC ambao wamepewa mafunzo ya kutosha na jinsi ya kuzitumia simu hizo.

“Niwaombe Watanzania kuitumia fursa hii vizuri, kwa kuuliza maswali ya msingi na si kufanya fujo. Pia simu hizo zimeunganishwa mitambo maalum kwa ajili ya kumtambua mpigaji simu, kutambua eneo alipo pamoja kurekodi mazungumzo,” anasema Kailima.

Msemaji wa UNDP, Awa Dabo amesema wameamua kudhamini mawasiliano hayo ili kudumisha urafiki uliopo baina yao na NEC na kuufanya uchaguzi mkuu uwe wa uwazi na haki.

“Tunajivunia kuwa wadhamini kwa mara ya pili sasa ikiwa na mwaka 2010 pia tulidhamini huduma hii. Najua kwa kipindi hiki cha kuelekea mwishoni wananchi wengi wanakuwa na maswali mengi ambayo yanaitaji kujibiwa kwa wakati na kwa weledi mkubwa,” amesema Dabo.

error: Content is protected !!