August 15, 2022

Uhuru hauna Mipaka

NEC: Mchakato Katiba Mpya upo palepale

Spread the love

DAMIAN Lubuva, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) amesema, mchakato wa kura za maoni na Katiba Mpya upo palepale, anaandika Hamisi Mguta.

Akizungumza leo mbele ya waandishi wa habari wakati akikabidhi Taarifa ya Uchaguzi Mkuu kwa Rais John Magufuli, Lubuva amesema, kilichobadilika ni muda na tarehe tu.

Amesema, kuahirishwa kwa mchakato huo kulitokana na zoezi la kuandikisha wapiga kura ambalo ndio msingi wa kukamilika kwa uchaguzi.

Sababu nyingine aliyotaja ni muingiliano wa zoezi hilo zito kwenda sambamba na mchakato wa Uchaguzi Mkuu.

“Kwa namna ya utani wanasema mzigo mzito mpe Mnyamwezi, lakini mizigo miwili hata kwa Myamwezi mwenyewe atashindwa,” amesema.

Amesema, mara nyingi watu wamekua wakiulizia suala hilo na wengine kuliongelea katika muktadha usio sahihi.

Amefafanua kuwa, “kura ya maoni haikuachwa bali ilisitishwa tu hivyo NEC na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) pia watasimamia kuhakikisha mapendekezo ya marekebisho yanafikishwa serikalini kwa utaratibu hatimaye muswada ufike bungeni.

“Kwa kuwa tulisema kwamba, kura za maoni ni baada ya kuisha kwa Uchaguzi Mkuu, sasa tume inaweza kujielekeza katika majukumu yake mengine,”amesema.

Tarehe 2 Aprili mwaka jana NEC ilitangaza kuahirisha mchakato wa kura za maoni baada ya Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete kukabidhi Tume ya Katiba inayopendekezwa na baadaye kueleza kuwa, mchakato huo ungekamilika 30 Aprili mwaka huo huo lakini kutokana na sababu zilizotajwa, mchakato huo haukufanyika.

error: Content is protected !!