December 3, 2022

Uhuru hauna Mipaka

NEC kuzindua uandikishaji wapiga kura Julai 18

Mwenyekiti wa NEC, Jaji Semistocles Kaijage

Spread the love

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), inatarajia kuzindua Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura tarehe 18 Julai 2019 mkoani Kilimanjaro. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Kwa mujibu wa taarifa hiyo imetolewa leo na NEC, inaeleza kwamba Jaji Semistocles Kaijage, Mwenyekiti wa NEC amefungua mkutano wa wadau unaofanyika mkoani Kilimanjaro, ikiwa ni maandalizi ya uzinduzi rasmi wa daftari hilo.

Taarifa hiyo ya NEC imeeleza kuwa, miongoni mwa wadau wanaoshiriki katika mkutano huo ni pamoja na wawakilishi wa vyama vya siasa, viongozi wa dini, wawakilishi wa watu wenye ulemavu, vijana na asasi mbalimbali za kiraia.

Wakati huo, Jaji Mbarouk Salumu Mbarouk,  Makamu Mwenyekiti wa NEC amefungua mkutano wa wadau mkoani Arusha, pia mkutano huo umeshirikisha wadau kutoka vyama vya siasa, asasi za kiraia na watu wenye ulemavu.

error: Content is protected !!