January 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

NEC: Hakuna goli la mkono

Spread the love

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema, Watanzania na wanasiasa nchini hawana sababu ya kuwa na wasiwasi kwa kuwa, hakutakuwa na goli la mkono. Anaandika Yusuph Katimba … (endelea).

“Ni uchokozi tu, hakutakuwa na goli la mkono zipo sheria, taratibu na kanuni na hizi ndio zitakazofuatwa. “Kwenye Tume ya Uchaguzi hakuna goli la mkono, vyama vyote visiwe na wasiwasi.

“Huku hakuna njia ya mkato. Nilisema, wanaosema kura zitaibiwa, watuambie ili tuzibe mianya hiyo,” amesema Mwenyekiti wa NEC, Jaji Mstaafu, Damian Lubuva leo jijini Dar es Salaam alipokutana na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari.

Akizungumzia maandalizi ya Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu Lubuva amesema maandalizi yanaendelea. “Mpaka tarehe 15 mwezi huu vifaa vyote tunatarajia view vimefika katika maeneo husika,” amesema.

Hata hivyo amevikumbusha vyama vya siasa kukumbuka kuzingatia maadili ili kuepusha nchi na ghasia zozote zinazoweza kutokea.

“Maadili yatawale katika uchaguzi mkuu. Kila chama kikizingatia maadili, sheria na kanuni za uchaguzi amani itaendelea,” amesema na kuongeza;

“Vyama vyote view tayari kuzingatia sheria na mshiriki yoyote awe tayari kukubali matokeo ya uchaguzi yatakayotangazwa na tume.”

Akizungumzia watu ambao hawataona majina yao kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kwa njia ya kielekroniki (BVR), Kamishna wa NEC, Jaji John Mkwawa amesema busara itatumika ili kupata haki hiyo.

“Tumepitia na tumeshughulikia kwa kiasi kikubwa. Ukifika kwenye kituo na hati ya kupigia kura, itatazamwa ili kuangalia uhalali wake na baada ya hapo hekima itatumika ili mtu huyo asikose haki yake ya kupiga kura,” amesema.

Katika hilo Jaji Lubuva aliongeza kuwa lengo zima la uhakiki ni kujua ni wapi kuna tatizo na kwamba, watu wa namna hiyo wakiwepo watapata msaada na wataweza kupiga kura.

Hata hivyo Jaji Lubuva amevitaka vyombo vya habari kusimamia maadili ya uandishi ili kutoa usawa na kuwatendea haki wananchi pamoja na wagombe wa vyama mbalimbali vya siasa nchini.

“Kwenye uchaguzi haitakiwi kuegemea popote. Mtakuwa hamjawatendea haki wananchi kama mtaegemea upende mmoja,” anasema Jaji Lubuva na kuongeza;

“Ili kila watu ashiriki Tume ya Uchaguzi inaomba kuhamasisha wananchi kwa ujumla. NEC inaomba kutumia kalamu ili watu waone umuhimu wa kutunza kadi zao.”

Jaji Lubuva alilalamika kwamba wakati wa kuandika wapiga kura kwenye BVR, waandishin walikuwa wakiripoti habari alizoziita kuwa hasi ikiwa ni pamoja na upungufu wake.

Hata hivyo, Katibu wa Jukwaa la Wahariri nchini (TEF), Nevile Meena alimweleza Jaji Lubuva kuwa, vyombo vya habari vilijitahidi kuonesha kasoro hizo ambazo baadaye walizifanyia kazi na kuwa, angepongeza kazi hiyo.

error: Content is protected !!