Saturday , 25 March 2023
Home Kitengo Michezo Ndumbaro mgeni rasmi Simba dhidi ya Platinum
Michezo

Ndumbaro mgeni rasmi Simba dhidi ya Platinum

Spread the love

WAZIRI wa Maliasili na Utalii, Dk. Damasi Ndumbaro, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mchezo wa klabu bingwa barani Afrika, kati wenyeji Simba Sport Club na Fc Platinum, kutoka Zimbabwe.  Anaripoti Kelvin Mwaipungu… (endelea).

Mchezo kati ya miamba hiyo miwili ya soka katika bara la Afrika, umepangwa kufanyika kwenye uwanja wa Benjamini Mkapa, jijini Dar es Salaam, kesho Jumatano, majira ya saa 11 jioni.

Simba na Fc Platinum zinakutaka katika mchezo wa marudiano, ambako katika mchezo wa kwanza uliochezwa nchini Zimbabwe 23 Desemba mwaka jana, Simba ilikubali kipigo cha bao moja bila majibu.

Katika mchezo huo, Simba watahitaji ushindi wa tofauti ya mabao kuanzia mawili, ili iweze kufuzu kwenye hatua ya makundi ya michuano hiyo.

Kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii, klabu ya Simba imethibitisha uwepo wa waziri huyo ambaye alishawahi kuwa Mwenyekiti wa kamati ya Rufani na Leseni ya TFF.

Ndumbaro, anayefahamika kama mwanasoka mbobezi na bingwa wa fitina za mpira wa miguu nchini, anatarajiwa kuongoza mashabiki takribani 30000 kuwapa sapoti wachezaji wa Simba pamoja na benchi la ufundi ili waweze kushinda mchezo huo.

Kwa mujibu wa taarifa za ndani ya klabu hiyo, Simba wanatarajiwa kukosa huduma za kiungo wake mahiri, Jonas Mkude ambaye amesimamishwa kutokana na utovu wa nidhamu.

Klabu ya Simba, imepanga kupeleka shauri linalomhusu mchezaji huyo machachari wa kiungo, kwenye kamati yake ya nidhamu.

Wachambuzi wa masuala ya michezo nchini wanasema, kwa jinsi Simba ilivyojiandaa katika mchezo huo wa kesho, hakuna namna ambayo Wazimbabwe hao wanaweza kuchomoka.

“Simba ni timu nzuri na imebobea katika michezo ya kimataifa,” ameeleza mmoja wa washabiki wa mpira nchini na kuongeza, hivyo basi, hakuna uwezekano wowote wa kushindwa kushinda pambano hilo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Yanga: Fedha za Rais Samia zinaleta ari kubwa

Spread the loveUONGOZI wa klabu ya Yanga, umesema fedha zinazotolewa na Rais...

Michezo

Simba Sc. yamvulia kofia Rais Samia, yamuahidi makubwa dhidi ya Horoya

Spread the loveWAKATI timu ya Simba ikiibuka na ushindi wa bao 3-0...

Michezo

Taasisi ya TKO na TFF yawapiga msasa makocha wa kike 54

Spread the love WAKATI Soka la wasichana likichipua kwa kasi Taasisi ya...

Michezo

Kimwanga CUP yazidi kutimua vumbi

Spread the loveMASHINDANO ya mpira wa miguu ya Kimwanga CUP ya kuwania...

error: Content is protected !!