Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Ndugai: Sitagombea ubunge 2025
Habari za SiasaTangulizi

Ndugai: Sitagombea ubunge 2025

Aliyekuwa Spika wa Bunge, Job Ndugai
Spread the love

 

MWANASIASA mkongwe na Spika mstaafu nchini Tanzania, Job Ndugai ametangaza kutogombea tena nafasi ya ubunge wa Kongwa mkoani Dodoma katika uchaguzi mkuu ujao 2025. Anaripoti Danso Kaijage, Dodoma … (endelea).

Ngugai ambaye amekuwa mbunge wa jimbo hilo kwa kipindi cha miaka 20 na kushika nafasi mbalimbali kama mwenyekiti wa Bunge, Naibu Spika na baadaye Spika, ametangaza uamuzi huo leo Jumapili tarehe 8 Mei 2022.

Ametangaza uamuzi huo miezi Micha che kupita tangu alipojiuzulu Uspika tarehe 6 Januari 2022, baada ya kauli yake kuhusu Serikali kuendelea kukopa nje ya nchi kuibua mjadala na kushinikizwa na viongozi wa chama chake- Chama Cha Mapinduzi (CCM) kujiuzulu.

Mara baada ya kujiuzuli CCM iliendesha mchakato wa ndani na aliyekuwa naibu spika, Dk. Tulia Ackson akapitishwa kuwania nafasi hiyo kisha akachaguliwa na wabunge kuwa Spika.

Leo Jumapili, tarehe 8 Mei 2022, akizungumza kwenye ibada ya kuweka wakfu gari ya Pareshii ya Mtakatifu Michael Kanisa Aglikan Tanzania Dayosisi ya Mpwapwa, Ndugai ametangaza uamuzi huo.

“2025 sitagombea nafasi ya ubunge tena nastaafu siyo kama nastaafu kwa kushindwa lakini ni jamabo ambalo tayari nilishalipanga muda mrefu uliopita hivyo tutaendelea kushirikiana kama ambavyo tunashirikiana sasa,” amesema Ndugai.

Kuhusu gari hiyo iliyonunuliwa kwa kuchangisha michango kwa wanumi wa kanisa hilio pamoja na watu mablimbali amesema anapongeza wote ambao wamehusika kupatikana kwa gari hiyo.

“Tunapaswa kufanya vitu vyetu wenyewe bila kutegemea mtu aje kutusaidia kwani hata maandiko yanasema tutakula kwa jasho lakini siyo kwa dezo kama yapo maandiko hayo basi inabidi viongozi wa dini waanze kutufundisha lakini mimi sijawahi kuyaona,” amesema

Aidha, amesema Watanzania wanapaswa kuondokana na habari ya kutegemea mtu kuja kuwafanyia mambo yao.

Naye Askofu wa Kanisa Aglikan Tanazania Dayoyosisi ya Mpwapw, Jacob Chimeledya, amesema ni aibu kuendelea kutegemea wahisani katika kila jambo.

“Ni aibu sisi Watanzania tulivyo na rasilimali za kutosha kuendelea kusubilia wahisani kutoka nje kufanyia mambo yetu ni aibu pia kiongozi wa serikali kuitangaza Tanzania kuwa ni masikini licha ya uwepo wa rasilimali za kutosha'” amesema Askofu Chimeledya.

Job Ndugai, wakati akiwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Kwa upande wake, Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Antony Mtaka aliwapongeza waliofanikisha kupatikana kwa gari hiyo ambayo itatumika na kasisa hilo kutatua chanagmoto za usafiri kila linapo hitajika.

Mtaka alisema jambo ambalo limefanywa na waumini hao kununua gari bila kusubiri msaada ni jambo lakuigwa na watu wote.

“Lazima sisi kama waumini tuache kitu ambacho tutaendelea kukumbukwa na kanisa na kuwapa wepesi viongozi wa dini katika mahubiri yetu siyo kutunga uongoo kwenye maziko yetu,” alisema

Aidha, aliwataka vingozi wa dini kutumia nyumba zao za ibada kuelimisha masula mbalimbali ya kijamii ikiwemo zoezi la sensa ya watu na kamazi itakayofanyika tarehe 23 Agosti 2022.

“Tanawashukuru viongozi wa dini kwa kutupa ushirikiano katika mambo mbalimbali ikiwemo wakati wa chanjo ya UVIKO-19 na sasa tunapokwenda kwenye sensa tunaoamba ushirikiano wenu wa kutosha kufanikisha zoezi hili,” alisema Mtaka

3 Comments

  • Ni busara na mazoea mazuri kuhakiki maandiko yenu kabla ya kuyatoa kwa wasomaji. Kuna makosa mengi ya kiuandishi ambayo yanaonyesha mwandishi huyu si makini.

  • Makosa yako wapi?
    Hoja za kupinga makosa ziko wapi?
    Ni rahisi kubomoa kuliko kujenga.

  • Ndugai hongera kwa uamuzi huo,serikali ya mama samia ni ngumu haswaa,inahitaji wanaofanana nae

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

Habari za Siasa

CCM yakemea ufisadi, yaipa kibarua TAKUKURU

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimekemea vitendo vya ubadhirifu wa...

Habari za Siasa

Bajeti ya Ikulu 2024/25 kuongezeka, bunge laombwa kurudhia Sh. 1.1 trilioni

Spread the love  WIZARA ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa...

error: Content is protected !!