Tuesday , 5 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Ndugai kama Magufuli, hataki kuguswa
Habari za Siasa

Ndugai kama Magufuli, hataki kuguswa

Job Ndugai,. Spika wa Bunge la Tanzania
Spread the love

SPIKA wa Bunge Job Ndugai ameagiza Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ulinzi na Usalama, kuhakikisha inamsaka mbunge wa Ubungo Saed Kubenea (Chadema) na kumfikisha katika kamati hiyo kesho, anaandika Dany Tibason. 

Mbali na Spika kumtaka mbunge huyo kufikishwa katika kamati hiyo pia mbunge mwingine ambaye ametakiwa kufika katika Kamati ya  ya Kudumu ya Bunge ya Kinga na Maadili ya Bunge ni Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe (ACT-Wazalendo) kwa kosa la kumlalamikia Spika kuwa hakuweza kupeleka taarifa za kamati alizoziunda kwa ajili ya kuchunguza biashara ya madini ya almasi na tanzanite.

Ndugai amesema kuwa matibabu ya Lissu yanaendelea vizuri na anaendelea kutibiwa kwa awamu licha ya kuwa maumivu ni makali kutokana na majeraha ambayo aliyapata huku akiwasisitiza watanzania pamoja na  kuendelea kumuombea ili aweze kupona haraka.

“Hali ya ndugu yetu,  mbunge mwenzetu Tundu Lissu inaendelea vizuri namadaktari wanampa huduma, majeraha yanataka oparesheni kadhaa, lakini anaendelea vizuri licha ya kuwa maumivu ni magumu, lakini tuendelee kumuombea “ amesema

“Kubenea kafedhehesha taasisi na mimi mwenyewe , naagiza Kamati ya Mheshimiwa Adadi imuite ili isaidie kamati juu ya Tundu Lissa, Kubenea alitumia madhabahu ya Mungu kusema uongo na kunituhumu mimi Spika kuwa nimesema uongo nimelidanganya Bunge na nimelidanganya taifa,” amesema

“Pamoja na kusema kuwa nimelidanganya Bunge na kusema Spika muongo sasa naiagiza kamati ya mheshimiwa Adadi kumuita mara moja tena kesho ili aje athibitishe kwa kusema madhabahuni  mbali na kumuita katika kamati ya ulinzi na usalama pia apelekwe kwenye kamati ya maadili na kamati zote mbili zishughulikie tena kwa haraka” aliagiza
Spika Ndugai.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Baba yake Ole Sabaya ashinda Uenyekiti CCM – Arusha

Spread the loveLoy Thomas Sabaya ambaye ni Baba wa aliyekuwa Mkuu wa...

Habari za Siasa

Serikali yaagiza uchunguzi chanzo maporomoko Hanang

Spread the loveSERIKALI imeagiza uchunguzi ufanyike ili kubaini chanzo cha maporomoko ya...

Habari za SiasaTangulizi

Maafa Manyara: Rais Samia akatisha ziara yake Dubai

Spread the loveRAIS wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, amekatisha ziara yake...

Habari za SiasaTangulizi

Wataalaam wa miamba watua Hanang

Spread the loveWaziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na...

error: Content is protected !!