Saturday , 20 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Ndugai awapa ‘makavu’ wabunge viti maalum
Habari za Siasa

Ndugai awapa ‘makavu’ wabunge viti maalum

Spika wa Bunge, Job Ndugai
Spread the love

JOB Ndugai, Spika wa Bunge amehoji wabunge wanawake wa viti maalum kwamba, katika uwakilishi wao bungeni, wamefanya kitu gani muhimu kusaidia wanawake wanaodhulumiwa? Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Spika Ndugai ametoa kauli hiyo leo tarehe 18 Juni 2019, bungeni Jijini Dodoma baada ya Silafu Jumbe Maufi, Mbunge Viti Maalum kuhoji kwamba, serikali ina mkakati gani wa kutatua changamoto za wajane kudhulumiwa mirathi?

Spika Ndugai aliutumia nafasi hiyo kuwashauri wabunge hao kutumia vyema kanuni za bunge, katika kutatua changamoto zinazowakabili wanawake wenzao ikiwemo kuunda miswada kwa ajili ya kurekebisha sheria au kuondoa changamoto zao, badala ya kuitegemea serikali peke.

Huku akigusia changamoto ya baadhi ya wajane kudhurumiwa mirathi na wengine kufukuzwa kwenye makazi yao, Spika Ndugai amewataka wabunge wanawake kutumia vyema mikutano ya bunge, iliyosalia kuunda miswada itakayowezesha kurekebisha sheria kandamizi kwa wanawake na au kukomesha ukatili wa kijinsia dhidi yao.

“Waheshimiwa wabunge, swali hili ni muhimu, hebu kwa mikutano mitatau iliyobaki kwa nyie wanawake wote muunde muswada fulani wa kwenu wenyewe.

“Rekebisheni haya mambo msisubiri serikali peke yake, tumieni njia mbalimbali zilizoko katika kanuni zetu. Hebu fanyeni jambo moja kwa wanawake, kwa mfano iwe marufuku katika nchi yetu  kufukuzwa katika nyumba za familia, au mambo haya ya mirathi wanahangaika kweli wanateseka na nyie ndio wabunge wao katika kipindi cha miaka mitano mmefanya nini cha kubadilisha maisha yao au kitaishia hivi hivi tu?  wabunge viti maalum, tufanye kitu.”

Balozi Augustine Mahiga, Waziri wa Katiba na Sheria amesema, changamoto ya wanawake kudhulumiwa mirathi inatokana na jamii hususan maeneo ya vijijini kukosa uelewa kuhusu sheria ya mirathi.

Kutokana na changamoto hiyo, Balozi Mahiga ameametoa wito kwa wabunge kuchangia jitihada za serikali katika kufikisha elimu ya mirathi kwa umma, huku akiahidi wizara yake kundaa mkakati utakaoshirikisha majaji, mahakimu viongozi wa mikoa na wilaya wa kutokomeza changamoto hiyo.

“Mimi naungana mkono na kina mama, kwa kweli katika utekelezaji wa sheria ya mirathi si tu wanasumbuliwa lakini wanabaguliwa, tatizo hili linaonesha kadiri tunavyokuwa mbali na miji hasa kina mama wa vijini.

“Nakubalina kwamba, mbali ya elimu hiyo, kuna haja ya kuwa na mkakati maalum ambao hata wizara yangu, majaji na hakimu watakuwa wanaelezwa na kushirikiana na utawala kwa ujumla katika mikoa na wilaya, pendekezo hili nitalipa kipaumbele, katika wizara yangu,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari za Siasa

Mavunde aagiza Perseus kuharakisha fidia Sengerema

Spread the loveWaziri wa Madini, Anthony Mavunde ameipongeza Kampuni ya Perseus kwa...

Habari za Siasa

Kigogo Chadema awanyooshea vidole vigogo serikalini kuhusu ripoti ya CAG

Spread the love  MWANACHAMA wa Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Boniface Jacob, amedai...

Habari za Siasa

Wabunge waikalia kooni TAKUKURU Bungeni

Spread the love  BAADHI ya wabunge wamelia na changamoto za utendaji wa...

Habari za SiasaTangulizi

Mpina ataka Waziri Majaliwa ajiuzulu, akosoa teuzi za mawaziri

Spread the love  MBUNGE wa Kisesa, Luhaga Mpina, amemtaka Waziri Mkuu, Kassim...

error: Content is protected !!