Friday , 29 March 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Ndugai awakumbatia Mdee, wenzake 18, ananga Chadema
Habari za SiasaTangulizi

Ndugai awakumbatia Mdee, wenzake 18, ananga Chadema

Halima Mdee
Spread the love

 

SPIKA wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai, ameendelea kuwakingia kifua waliokuwa wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Halima Mdee na wenzake 18 akisema, hawezi kuwafukuza “kwa kipeperushi cha barua.” Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Mdee na wenzake, bado wanahudumu kama wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, pamoja na kufutwa uanachama wa vikao halali vya chama hicho.

Akizungumza bungeni mjini Dodoma, leo Jumatatu, tarehe 3 Mei 2021, Ndugai alisema, “…mimi ni spika mzoefu, nimekuwa hapa bungeni miaka 20, wako watu wanapiga kelele, Ndugai amevunja katiba.”

Alisema, “katibu yoyote anayeniandikia barua yenye mgogoro, usiniandikie kipeperushi tu. Aandike barua, aambatanishe na katiba yake, aniambatanishie na muhtasari wa hicho kikao, yawezekana huyo katibu mkuu amendika tu huko.”

Kundi hilo la wabunge 19, lililopachikwa jina la Covid 19, lilifukuzwa uanachama wa Chadema na Kamati Kuu (CC), iliyokutana tarehe 27 Novemba 2021.

Walituhumiwa kwa makosa mbalimbali yakiwamo usaliti, kughushi nyaraka za chama, uchonganishi, kutengeneza migogoro, ubinfasi na kujipeleka bungeni kujiapisha kuwa wabunge wa viti maalum, kinyume na maelekezo ya chama.

Mara baada ya uamuzi huo, Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika alimwandikia Spika Ndugai, barua ya kumjulisha maamuzi hayo ya kumfukuza Mdee uanachama wa chama hicho na hivyo, kupoteza sifa za kuwa wabunge.

Hata hivyo, kwa nyakati tofauti, Spika Ndugai amekuwa akiwakingia kifua kundi hilo na kusema, anawatambua kuwa wabunge wa Chadema na kuwataka waendelee kufanya kazi.

Taarifa ya Spika kuwa amepokea barua ya Chadema, lakini amegoma kuifanyia kazi kwa kuwa ni “kama kipeperushi,” inatofautiana na ile iliyotolewa na Naibu Spika wa Bunge, Tulia Ackson Mwansasu, kwamba Bunge halijawahi kupokea barua ya kuwavua unachama Mdee na wenzake.

Dk. Tulia alieleza hayo, kujibu maelezo ya Jesca Kishoa, mmoja wa wabunge waliofukuzwa uanachama wa Chadema, kuwa Bunge halijapokea taarifa hiyo.

Kishoa alieleza Bunge, kwamba ni kweli kuwa yeye na wenzake wamefutwa uanachama wa chama hicho.
Aidha, wakati Ndugai akitaka kumbukumbu za vikao vya Chadema, Machi mwaka 2017 aliridhia kufutwa uanachama kwa wabunge wanane wa Viti Maalum, kupitia Chama cha Wananchi (CUF), katikati ya mgogoro mkubwa wa uongozi, uliokuwa umekikumba chama hicho.

Kumbukumbu zinaonyesaha kuwa barua ya kuwafuta uanachama wabunge hao, iliandikwa na mwenyekiti wa chama hicho, Prof. Ibrahim Lipumba.

Vilevile, Spika Ndugai, aliwahi kurishia kufutwa uanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), aliyekuwa mbunge wa Viti Maalum na mwenyekiti wake wa Umoja wa Wanawake (CWT), Sophia Simba.

Ndugai alifanyia kazi barua zote za CCM na CUF, bila kuhoji maamuzi ya vikao vilivyoamua kufutia uanachama wabunge hao.

Job Ndugai Spika wa Bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania

Kwa mujibu wa maelezo ya Ndugai, kuhusiana na “sakata la Mdee na wenzake,” mara baada ya kupokea baarua hiyo, ataipeleka kwa watu wake wa sheria, ili kuiangalia kama imekidhi vigezo.

Alisema, “Je, sawa sawa, hawa wajumbe wa kamati kuu waliokaa ndiyo hawa? Namuuliza msajili, naangalia kwenye muhtasari. Hawa waliotuhumiwa walipata muda wa kusikilizwa? Nafukuzaje watu ambao hawakusikilizwa kokote.”

Akiendelea kuwatetea, Spika Ndugai amesema, “vipo vyama vimejaa mfumo dume, wapo watu wanakaa wanafukuza watu 19 kwa mpigo tena wanawake, kwa barua tu tena kipeperushi!

“Katiba yao, ina mambo ndani yake, wamechukua hatua za ndani ya Katiba yao, kwa katiba yao kuna Baraza Kuu, hilo Baraza Kuu limekutana, limefanya uamuzi wa mwisho?”

Huku akishangiliwa, Spika Ndugai alisema, “endeleni kuchapa kazi, msiwe na wasiwasi, mko mikono salama.” Haijapangwa spika achukue hatua siku mbili, siku nne, kwa nini watu wananiingilia, tutafika tu,” alisema.

Kiongozi huyo wa Bunge alisema, “tabia ya kuonea wanawake lazima iishe katika nchi hii, kwa kupambana na baadhi ya vyama kama hiki cha ajabu ajabu. Nani asiyejua hawa mabinti waliovyopambana?”

Mbali na Mdee, ambaye alikuwa mwenyekiti wa baraza la wanawake wa Chadema (Bawacha), wengine waliofutwa uanachama, ni waliokuwa wajumbe wa Kamati Kuu, Ester Bulaya na Esther Matiko; aliyekuwa katibu mkuu wa Bawacha, Grace Tendega na aliyekuwa makamu mwenyekiti (Bara), Hawa Subira Mwaifunga.

Katika orodha hiyo, wamo pia Agnesta Lambat, aliyekuwa katibu mwenezi wa Bawacha; Asia Mwadin Mohamed, aliyekuwa naibu katibu mkuu wa Bawacha Zanzibar; Jesca Kishoa, aliyekuwa naibu katibu kuu wa Bawacha (Bara) na aliyekuwa katibu mkuu wa Baraza la Vijana (Bavicha), Nusrat Hanje.

Wengine, ni aliyekuwa mwenyekiti wa Chadema mkoani Mtwara, Tunza Malapo; Cecilia Pareso, Naghenjwa Kaboyoka, Sophia Mwakagenda, Kunti Majala, Salome Makamba, Anatropia Theonest, Conchesta Lwamlaza, Felister Njau na Stella Siyao.

1 Comment

  • Mbona wao wenyewe wamesema hawana chama? Kama ni wanachama kwa nini wasioneshe kadi ya uwanachama na malipo ya ada?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Chadema: Samia aunde tume kuchunguza mauaji mgodi wa Barick

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, ameombwa aunde tume huru kwa...

KimataifaTangulizi

Zuma akataliwa kugombea urais

Spread the love  TUME Huru ya Uchaguzi Afrika Kusini (IEC) imemwondoa rais...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Nani anasema kuna hasara ATCL?

Spread the loveRIPOTI za makusanyo na matumizi ya fedha katika Kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

CAG: Wastaafu, wenza wao chanzo NHIF kufilisika

Spread the loveRIPOTI ya ukaguzi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu...

error: Content is protected !!