Sunday , 3 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Ndugai awabagua wapinzani, wamtolea uvivu
Habari za SiasaTangulizi

Ndugai awabagua wapinzani, wamtolea uvivu

Job Ndugai,. Spika wa Bunge la Tanzania
Spread the love

SPIKA wa Bunge, Job Ndugai amewaagiza mawaziri kutopeleka fedha katika majimbo ya wapinzani kutokana na kuikataa bajeti kwa kupiga kura ya hapana, anaandika Dany Tibason.

Ndugai alitoa kauli hiyo baada ya kumalizika kwa upigani kura wa kupitisha bajeti, ambapo ilipita kwa kura za ndiyo 260 na 95 za hapana huku moja haikupigwa kutoka kwa wabunge 356 waliokuwa bungeni.

Kauli hiyo ya Ndugai iliahamsha hasira kwa wabunge wa upinzani ambao ndiyo waliopiga kura ya hapana na kudai kuwa spika anatumia kiti chake kwa upendeleo na kuikanyaga katiba na kanuni za bunge.

Hali hiyo ilileta mvutano mkali kati ya spika na wabunge hao, na kusababisha Ndugai kumwamru Mbunge wa Ukonga Mwita Waitara (Chadema) kutoka nje kwa madai ya kubishana na kiti.

Mbunge wa Vunjo, James Mbati amesema kuwa kutokana na uendeshaji wa bunge kwa sasa ni bora kurejesha mswada wa sheria bungeni ili kuweza kutengeneza sheria mpya ya kuwepo kwa chama kimoja cha siasa kuliko ilivyo sasa.

Mbatia amesema hayo kutokana na wabunge wengi wa CCM kudai kuwa wabunge wa Upinzani ambao wamepiga kura za hapana kana kwamba wamekiuka sheria au kutojua kile wanachokifanya.

Naye mbunge wa Momba, David Silinde amesema kauli ya spika ya kuwaelekeza mawaziri kutotoa huduma kwa wabunge wa upinzani waliopiga kura ya hapana ni ubaguzi wa waziwazi.

“Kauli kama hizi zinaweza kulipasua bunge na kuweza kuwagawa watanzania, mwanzoni alipokuwa akizungumza nilidhani kuwa alikuwa anatania, lakini kutokana na kuwepo kwa wabunge wasiojua wamebeba kauli hiyo kama ni agenda,” amesema Silinde.

Naye mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa (Chadema) amesema wabunge wote waliopo ndani ya ukumbi wa bunge ni wawakilishi wa watanzania waliowapigia kura.

Amesema kupigiwa kura huko siyo kwa bahati mbaya kwa maana hakuna mbunge yoyote ambaye yupo bungeni kwa bahati mbaya na wapo kwa ajili ya kuwawakilisha wananchi waliowatuma.

Hata hivyo Mchungaji Msigwa amesema wabunge au serikali isidhani kuwa upelekwaji wa fedha za katika majimbo siyo hisani kwani pesa hizo ni pesa za walipa kodi ambao ni watanzania ambao ni wapiga kura wa CCM na waliokuwa siyo wa CCM.

“Lazima mtambue maendeleo yameletwa na pande mbili ambazo zimekuwa zikitofautiana kwa mawazo na kupingana kwa hoja, lakini kwa siku hizi tano kiti cha spika kimekuwa na upendeleo mkubwa kwa kuonesha upendeleo wa wazi kwa kuwakandamiza wapinzani na kuwapa nafasi nyingi za upendeleo wabunge wa CCM,” amesema Mchungaji Msigwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

20 wafariki dunia kwa mafuriko Manyara

Spread the loveMVUA za vuli zinazoendelea kunyesha maeneo mbalimbali nchini zimeleta madhara...

Habari za Siasa

Dk. Biteko aagiza wakurugenzi TANESCO kukemea rushwa kwenye maeneo yao

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Uongozi wa Samia kuendelea hadi 2030

Spread the loveKWETU sisi tuliowahi kusoma sekondari, iwe O levo au A...

Habari za SiasaMakala & Uchambuzi

Bado askari wastaafu wanaonewa

Spread the loveRAIS wangu Samia Suluhu Hassan tunaendelea kumshukuru Mungu kwamba wote...

error: Content is protected !!