SPIKA wa Bunge Job Ndugai amewateua wabunge 15 kuwa wajumbe wa Kamati ya Kanuni za Bunge. Anaandika Josephat Isango … (endelea)
Kamati ya Kanuni imeundwa na kutangazwa kabla ya nyingine ili ifanye marekebisho na nyongeza kwenye kanuni za kudumu za Bunge kuhusu majukumu ya kamati zingine.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na na kitengo cha habari, Elimu na Mawasiliano cha Bunge kamati hiyo itakuwa na kazi ya kuhusianisha majukumu ya serikali kwa kuzingatia idadi ya sasa ya Wizara ili kutoa urahisi, ufanisi na tija kwa Bunge kuisimamia na kuishauri serikali.
Wabunge walioteuliwa ni pamoja na Tundu Lissu, Jasson Rweikiza, Dk Jasmine Bunga, Makame Kassim, Ally Saleh, Magdalena Sakaya, Salome Makamba, Zainab Katimba, Balozi Adadi Rajab, Charles Tizeba na Kangi Lugola.
Imebainishwa kuwa Kamati ya Kanuni za kudumu za Bunge itaongozwa na Mwenyekiti wake ambaye ni Spika, na Makamu mwenyekiti ni Naibu Spika, Tulia Ackson, pamoja na kiongozi wa Upinzani Bungeni (KUB) na Mwanasheria Mkuu (AG) ambao wanaingia katika kamati hiyo kwa nyadhifa zao
Spika anatarajiwa kukamilisha uteuzi wa wajumbe katika kamati nyingine kabla ya kuanza mkutano wa pili wa Bunge unaotarajiwa kuanza Januari 26 mwaka huu.
More Stories
Sakata la Mahindi Kenya Vs Tanzania: Zitto aonesha njia
COVID-19: Prof. Lipumba ‘watu wana hofu’
CCM ya tetea wazawa miradi ya ujenzi