Wednesday , 24 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Ndugai amwapisha anayekwenda kumrithi aliyeshindwa kuapa
Habari za Siasa

Ndugai amwapisha anayekwenda kumrithi aliyeshindwa kuapa

Aliyekuwa Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai
Spread the love

SPIKA wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai amemwapisha, Profesa Shukrani Manya kuwa Mbunge wa kuteuliwa na Rais. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Profesa Manya, aliyekuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini Tanzania, ameapishwa leo Ijumaa tarehe 11 Desemba 2020 na Spika Ndugai katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma.

Baadaye leo mchana, Profesa Manya ataapishwa na Rais wa Tanzania, John Magufuli kuwa Naibu Waziri wa Madini akichukua nafasi ya Francis Ndulane aliyeshindwa kuapa vizuri.

Ndulane ambaye ni Mbunge wa Kilwa Kaskazini Mkoa wa Lindi, alishindwa kuapa vizuri Jumatano ya tarehe 9 Desemba 2020, wakati Rais Magufuli alipowaapisha mawaziri 21 na naibu mawaziri 22 Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma.

Baada ya kuambiwa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi kurejea upya kuapa, alionekana kuweweseka ndipo, Balozi Kijazi alimweleza akapumzike kwanza huku Rais Magufuli akiahidi kuteua mtu mwingine “anayejua kuapa vizuri.”

Profesa Manya aliyezaliwa tarehe 5 Machi 1973, Ukerewe jijini Mwanza, amekuwa mbunge wa tano kuteuliwa na Rais kati ya nafasi kumi alizonazo Rais kwa mujibu wa Katiba.

Profesa Manya alishika nafasi ya Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini kuanzia mwaka 2018 huku akiendelea na Uhadhiri katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).

Wengine waliokwisha teuliwa na kuapishwa ni; aliyekuwa mbunge wa viti maalum kupitia CUF katika Bunge la 11 ambapo mwisho wa Bunge hilo alitangaza kurejea  CCM, Riziki Lulida pamoja na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole.

Wengine ni; Aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Tamisemi anayeshughulikia sekta ya afya, Dk. Dorothy Gwajima ambaye pia alimteua na kumwapisha kuwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.

Mwingine ni; Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano anayeshughulikia Uchukuzi, Dk. Leonard Chamriho ambaye alimteua na kumwapisha kuwa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi.

Mara baada ya kuteuliwa, Profesa Manya amemshukuru Mungu “kwani yeye ndiye hupanga majira na nyakati za mwanadamu. Nimeshukuru Rais Magufuli kwa kuniteua kuwa mbunge na nitafanya majukumu yangu ya ubunge kwa uadilifu ili kwa pamoja tulisukume gurudumu mbele la Taifa letu.”

Spika Ndugai amesema, wabunge wanne wa ACT-Wazalendo ambao bado hawajaapa kama wana nia ya kuitumikie nchi yao “kama kweli waliomba ubunge kuwatumikia wananchi, hawana sababu ya kuendelea kuzulula huko waliko, watoe taarifa haraka kwa spika, tuwapangie ili wapate kiapo waendelee kufanya kazi za kibunge kama wananchi walivyowaamini. Nadhani ni watatu.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mwekezaji amwaga bil. 39 kujenga viwanda 3 vya uchenjuaji

Spread the loveKampuni ya Mineral Access System Limited (MAST) inayoiwakilishwa kampuni ya...

Habari za SiasaTangulizi

Mpwa wa Magufuli mbaroni kwa kusambaza picha za utupu

Spread the loveJESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limewakamata...

Habari za Siasa

Serikali kuanzisha mradi wa Gridi ya maji ya Taifa

Spread the loveWaziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema katika mwaka wa fedha...

error: Content is protected !!