
Viongozi wa Chadema wakiweka shada la maua katika kaburi la Marehemu, Mwalimu Kasuku Bilago. Picha ndogo Spika wa Bunge, Job Ndugai
SPIKA wa Bunge la Jamhuri, Job Ndugai, amekituhumu Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kufuatia hatua yake ya kulizuia Bunge, kumzika mbunge wa Buyungu, Mwalimu Kasuku Bilago. Anaripoti Mwandishi Wetu kutoka Dodoma… (endelea).
“Nimefadhaishwa na kusikitishwa sana na uamuzi wa wabunge wa Chadema kunizuia mimi na Bunge, kutimiza wajibu wake wa msingi wa kumzika mbunge wake, Mwalimu Kasuku Bilago,” ameeleza Ndugai katika mazungumzo yake na mbunge mmoja kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM), ofisini kwake mjini Dodoma.
Amesema, “hawa watu ni wa ajabu sana. Hakukuwa na sababu yeyote ya msingi ya kugombana katika jambo hili. Lakini haya yametokea kutokana na kutokuwapo tu kwa mawasiliano.”
More Stories
Simba yaichapa Jkt, Yaisogelea Yanga
Dk. Mwinyi atoa fursa kwa wanahabari Z’bar
Rais Mwinyi ateua mrithi wa Maalim Seif