July 1, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Ndugai akalia kuti kavu jimboni

Mbunge wa Kongwa, Job Ndugai

Spread the love

WAZEE wa  Kata ya Lenjulu wilayani Kongwa mkoani Dodoma, wamemkataa mbunge wao Job Ndugai  badala yake wamewataka vijana, wanawake pamoja na wazee kuhakikisha wanajitokeza kupiga kura kwa ajili ya kukiondoa Chama Cha Mapinduzi CCM madarakani. Anaandika Dany Tibason … (endelea).

Ndugai ambae pia ni Naibu Spika wa Bunge wazee hao  hao wametangaza kumkataa  kwa madai kuwa amekuwa mbunge  mwenye ubaguzi wa kimaendeleo na wananchi wanakabiliwa na shida mbalimbali ikiwemo huduma za kijamii kwa miaka 15 ya uongozi wake.

Mzee aliyejitambulisha kwa jina la Chimola (98) amesema  kuendelea kuikichagua chama hicho tawala ni sawa na kusafiri na gari bovu ambalo linasukumwa kila mara.

Mzee huyo ambaye alikuwa akishangiliwa na umati wa watu katika mkutano wa hadhara kwa ajili ya mtangaza nia ya kugombea ubunge katika jimbo la Kongwa kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Esau Mgobei amesema  umefika wakati wa kubadilisha maisha na kufanya mageuzi.

Aidha, alienda mbali  na kusema iwapo vijana wanasema wazee wamepitwa na wakati umefika sasa wakati  vijana hao kukipumzisha chama hicho kwa kuwa  kimepitwa na wakati na sasa wanahitaji mabadiliko ya kweli.

“Nawashangaa vijana ambao mnafanya mzaa kwa kushindwa kuiondoa CCM madarakani kwa sasa ina miaka mingi ni kwanini isiondolewe madarakani ili watawale watu wengine.

“Siku hizi mnasema kuna magari mapya nay a kisasa kwa maana magari hayo yanatokana na viwanda vya kisasa, kwa maana hiyo basipandeni gari mpya kwa kumchagua mbunge wa Chadema ambaye anatokana na kiwanda kipya cha Chadema kupitia Ukawa” amesema  Chimola.

Nae  mzee Endson wakati wa kumvalisha migorole na kumpatia silaha  mbalimbali za kimila, mtangazania nia huyo amesema  wanamkabidhi ngao kijana huyo ili kuhakikisha anapambana na adui yake ambaye analishikilia jimbo hilo.

Kwa upande wake Mgobei amesema  sasa yatosha kuendelea kutawaliwa na CCM kutokana na chama hicho kuwabagua wananchi.

Amesema  wananchi wamekuwa masikini kutokana na uongozi mbovu wa CCM kwa kuwakumbatia wenye nacho na kuwatelekeza wale ambao ni walalahoi.

Amesema  ili kutambua uongozi wa CCM kuwa ni wa ubaguzi ni pale ambapo viongozi wa serikali wanalindana katika kashifa mbalimbali za ufisadi wa mali ya umma.

Aidha,amesema  iwapo atapata ridhaa ya kupeperusha bendera kwa ajili ya kuwania nafasi hiyo ya ubunge na kuchaguliwa kuingia bungeni jambo la kwanza ni kuhakikisha anaunganisha nguvu kwa wana Kongwa ili kuondoa umasikini wa kipato kwa familia.

Aliongeza kuwa  jambo pekee ambalo linaweza kuondoa umasikini ni pale ambapo ataunganisha nguvu kwa kushirikiana na wataalamu  wa kada mbalimbali.

Nae  Naibu Katibu Mkuu wa Baraza la Wanawake Chadema (BAWACHA) Kunti Majara aliwataka wanawake kuachana na ushabiki wa kuhongwa vilemba, mitandio na viongozi wa CCM ili wawapigie kura.

Hata hivyo amesema  wanaume  nao waepukane na kukubali kuvalishwa kapero na tisheti ikiwa ni pamoja na kuhongwa pombe ya kienyeji na badala yake watambue ukombozi pekee unatokana na vyama vya upinzani.

Katita mkutano huo ambao ulikuwa umesheeni wananchi naye Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Mkoa wa Dodoma (BAVICHA),Manyanya Malambaya Manyanya alisema iwapo vijana hawatakuwa tayari kupiga kura kwa ajili ya kuiondoa CCM madarakani ni wazi umasikini utaendelea kuwatesa watanzania.

Alisema watanzania wengi wanateseka kutokana na vijana kutojitokeza kupiga kura au kuhongwa na wagombea wa CCM kwa pesa ndogo ambayo inawatesa kwa kipindi cha miaka mitano.

error: Content is protected !!