Tuesday , 5 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Ndugai acharuka Bunge kuitwa dhaifu, ataka pingu zitumike
Habari za SiasaTangulizi

Ndugai acharuka Bunge kuitwa dhaifu, ataka pingu zitumike

Spika wa Bunge, Job Ndugai
Spread the love

SPIKA wa Bunge la Jamhuri, Job Ndugai, ameagiza kufika mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Haki, Kinga, Maadili na Madaraka, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Prof. Mussa Assad. Anaripoti Danson Kaijage, kutoka Dodoma … (endelea).

Aidha, Ndugai amemtaka mbunge wa Kawe, Halima James Mdee, kufika mbele ya kamati hiyo, tarehe 22 Januari mwaka huu.

Kwa mujibu wa Spika Ndugai, mbunge huyo wa Kawe (Chadema), anapaswa kufika mbele ya Kamati ya Bunge, kufuatia “kauli yake ya kuunga mkono msimamo wa Prof. Assad.”

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Jumatatu mjini Dodoma, Spika Ndugai amesema, Prof. Assad, anatakiwa kufika mbele ya kamati hiyo, tarehe 21 Januari 2019, ili kujibu “tuhuma za kudhalilisha Bunge.”

Amedai kuwa ameamua kuchukua hatua hiyo, baada ya kujiridhisha kuwa CAG alinukuliwa akisema, “Bunge la sasa ni dhaifu.”

Amesema, “…ninamtaka CAG, kufika mbele ya Kamati ya Haki, Kinga, Maadili na Madaraka ya Bunge, kwa hiari yake, tarehe 21 Januari mwaka huu. Akishindwa, nitaagiza akamatwe na kuletwa mbele ya kamati kwa nguvu.”

Prof. Assad alinukuliwa na Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa akisema, “Bunge limekuwa dhaifu na hivyo limeshindwa kuisimamia serikali katika masuala ya matumizi ya fedha za umma.”

Alikuwa akijibu swali aliloulizwa na mwandishi wa habari wa radio hiyo, kwamba kuwa kwa nini yeye (CAG) anafanya kazi nzuri, lakini baada ya ripoti yake kufikishwa bungeni, hakuna hatua zinazochukuliwa.

Akijibu madai hayo, Ndugai amesema, Bunge limepokea kwa masikitiko makubwa kauli hiyo ya CAG na kuongeza, “Bunge limefanya mambo mengi kutokana na kazi yake ya kuishauri na kuisimamia serikali.”

Amesema, “nataka kumhakikishia CAG kwamba sisi siyo dhaifu. Nakazia wito huu; kuwa Prof. Assad atokee mbele ya kamati, tarehe 21 Januari 2019. Nataka aje athibitishe kauli yake kuwa Bunge ni dhaifu.

Amesema, ofisi yake imesikitishwa kufanya kazi na mtu anayekuona ni taasisi dhaifu, sasa pamoja na kulindwa na Katiba, tunamshauri ajitathimini upya na hatutavumilia hata dakika moja kudharauliwa.

Amesema, kutokana na hali hiyo, anatumia mamlaka yake kwa mujibu wa Sheria ya za Tanzania, Sura ya 296 na kwa mamlaka aliyonayo kwa mujibu wa kifungu cha 4(a)(8) cha Kanuni za Kudumu za Bunge, kulipeleka suala hilo kwa Kamati ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge, ili wakalifanyie kazi na kisha kumshauri.

Alisema kauli ya Prof. Assad inatoa picha kama vile ripoti zake zikishatolewa bungeni kazi yake ndio inakuwa imekwisha jambo ambalo siyo kweli.

Amesema, “CAG na maofisa wake wanaingia bungeni wakati wowote kwenye kamati zetu za usimamizi. Ripoti zake zikishafika kwenye kamati, muda wote maofisa wake, wanakuwa pro ndani ya kamati ile na wanaeleza kilichotokea walipokagua. Hivyo kama kuna upotoshaji yeye na maofisa wake ndio watu hasa namba moja.”

Ndugai amedai kuwa licha ya Bunge kutekeleza wajibu wake wa kuisimamia Sserikali, lakini ripoti za ofisi za CAG hazina jambo lolote kubwa analodhani Bunge limeshindwa kulisimamia.

Katika hatua nyingine, spika huyo wa Bunge la 11 ametumia nafasi hiyo kuonya maofisa wa serikali, taasisi za umma, watu binafsi na wananchi wengine wa kawaida, kuwa Bunge halifurahishwi na kauli za kulidharau na kujaribu kulidhalilisha.

“Naomba ieleweke kuwa siyo kwamba hatupendi kukosolewa. La hasha. Tunachokikataa hapa, ni dharau. Ninyi waandishi ni mashahidi mnatukosoa kila kukicha, lakini hatugombani,” ameeleza.

SPIKA wa Bunge la Jamhuri, Job Ndugai, ameagiza kufika mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Haki, Kinga, Maadili na Madaraka, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Prof. Mussa Assad. Anaripoti Danson Kaijage, kutoka Dodoma.… (endelea).

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Dk. Biteko: Viongozi tuache alama nzuri katika utendaji wetu

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari za SiasaTangulizi

Chanzo maporomoko yaliyoua 65 Hanang, chatajwa

Spread the loveSERIKALI imesema kumeguka kwa sehemu ya Mlima Hanang ambao ilikuwa...

Habari za Siasa

Baba yake Ole Sabaya ashinda Uenyekiti CCM – Arusha

Spread the loveLoy Thomas Sabaya ambaye ni Baba wa aliyekuwa Mkuu wa...

Habari za Siasa

Serikali yaagiza uchunguzi chanzo maporomoko Hanang

Spread the loveSERIKALI imeagiza uchunguzi ufanyike ili kubaini chanzo cha maporomoko ya...

error: Content is protected !!