August 17, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Ndugai abariki timua timua ya Prof. Lipumba

Job Ndugai,. Spika wa Bunge la Tanzania

Spread the love

JOB Ndugai, Spika wa Bunge amebariki kuvuliwa uanachama kwa wabunge nane wa Chama cha Wananchi (CUF) na anayedai kuwa Mwenyekiti halali wa chama hicho, Prof. Ibrahimu Lipumba, anaandika Erasto Masalu.

Spika Ndugai amekubali barua aliyoandikiwa na Prof. Lipumba na Kaimu Katibu wake, Magdalena Sakaya ya kuwavua uanachama wabunge hao.

Kutokana na Spika Ndugai kukubali barua hiyo, wabunge Severina Silvanus Mwijage, Saumu Sakala, Salma Mwassa, Riziki Ngwali, Raisa Abdallah Mussa, Miza Bakari Haji, Hadija Ally Al-Qassmy na Halima Ali Mohamed wamekosa sifa ya kuwa wabunge.

Hatua hiyo inamaanisha kuwa Spika Ndugai anamtambua Prof. Lipumba kama Mwenyekiti halali wa CUF kama ilivyokuwa kwa msajiri wa vyama.

CUF wamekuwa na mgogoro ndani ya chama chao na tayari wana kesi mahakamani ya kutambua uongozi halali kati ya unaomtambua Prof. Lipumba na ule unaomuunga mkono Katibu wa chama hicho, Seif Sharrif Hamad.

error: Content is protected !!