May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Ndoa ya Ndayilagije na TFF yafikia mwisho

Clifford Ndimbo, Msemaji wa TFF

Spread the love

 

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imevunja rasmi mkataba na aliyekuwa kocha wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Etienne Ngayilagije baada ya kukubaliana kwa pande zote mbili. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Ettiene alikuwa anakinoa kikosi cha Taifa Stars baada ya kuchukua mikoba kutoka kwa Emannuel Amunike aliyetimuliwa kwa kufanya vibaya kwenye michuano ya kombe la Mataifa Afrika (AFCON) 2019 yaliyofanyika nchini Misri.

Taarifa kutoka TFF iliyotolewa muda mfupi hii leo tarehe 11 Februari 2021, imeleza kuwa pande zote mbili zimefikia makubaliano hayo baada ya kikao cha pamoja.

Aidha taarifa hiyo imeeleza kuwa mchakato wa kumapata mbadala wa Ndayilagije utaanza hivi karibuni ili kurithi nafasi yake.

Pengine kufanya vibaya kwenye michuano ya kombe la Mataifa Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN) kwa Taifa Stars ndio sababu kubwa ya kuondolewa kwa kocha huyo.

error: Content is protected !!