May 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Ndoa ya Mbunge, mtoto wa Mbunge yaingia mdudu

Spread the love

 

NDOA ya Mbunge wa Korogwe Vijijini (CCM), Timotheo Mnzava na mchumba wake, Caroline Pallangyo, ambaye ni mtoto wa Mbunge wa Arumeru Mashariki, John Pallangyo, imeingia mdudu baada ya kuwekewa pingamizi Kanisani la Kiijili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Usharika wa Mombo, Tanga. Anaripoti Mwandishi Wetu, Tanga … (endelea).

Ndoa hiyo inayotarajia kufungwa tarehe 10 Julai 2021, imewekewa pingamizi na mwanamke anayefahamika kwa jina la Anna, anayedai kuishi naye na kuzaa naye, kabla ya kuamua kufunga ndoa na mwanamke mwingine kwa kificho.

Mwanamke huyo anayeishi Dodoma kikazi, ambaye ni mtumishi wa Serikali anasema, amebahatika kupata naye mtoto mmoja. Na walianza uhusiano walipokutana Tanga alikokwenda kikazi.

Undani wa habari hii kujua nini kimetokea kanisani baada ya pingamizi hilo, baba mkwe alichokisema, bwanaharusi mwenyewe na maelezo ya kina ya Anna, soma Gazeti la Raia Mwema, toleo la leo Jumatatu, tarehe 28 Juni 2021.

error: Content is protected !!