August 16, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Ndoa chini ya miaka 18 marufuku

Mahakama Kuu ya Tanzania

Spread the love

 

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam jana imebatilisha sheria ya ndoa ya mwaka 1971 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002 iliyokuwa inatoa mwanya wa binti wa  chini ya umri wa miaka 18 kuolewa, anaandika Faki Sosi.

Kesi hiyo ilifunguliwa na Rebeca Gyumi, Mkurugenzi wa Msichana Initiative, shirika lisilo la serikali linalofanya kazi ya kutetea haki za watoto wa kike kupata elimu, kupitia wakili Jebra Kambole.

Kesi hiyo namba 5 ya mwaka 2016 ambapo walalamikaji katika kesi hiyo walikuwa wanapinga  kifungu cha 13 na 17 vya sheria ya ndoa (CAP 29 R.E 2002) kwa kutoa mwaya kwa mtoto wa kike kuolewa akiwa na miaka 14 kwa kibali cha mahakama, na miaka 15 kwa ridhaa ya wazazi.

Kifungu cha 17 kinachotoa ruhusa kwa mtoto wa kike kuolewa akiwa na miaka 15 kwa ridhaa ya wazazi, kina minya utu na haki ya mtu kujieleza kama zilivyoainishwa kwenye Ibara ya 12 na 18 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano.

Masuala ya ndoa si kama mikataba ya biashara, pande zinazoingia kwenye ndoa lazima zikubaliane na si kulazimishwa. Na tumeona hata matukio ambapo wazazi walikatiza mtoto wa kike masomo ili aolewe.

Hukumu ya kesi hiyo imetolewa na Shaban Lila Jaji Kiongozi katika Mahakama hiyo wengine ni Jaji Sekiet na kwamba mahakama imebatilisha kifungu kilichokuwa kinahalalisha ndoa za binti kuolewa akiwa chini ya umri wa miaka 18.

 

error: Content is protected !!