January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Ndesamburo aivuruga Chadema

Spread the love

MGOGORO wa kura za maoni za kutafuta mgombea ubunge jimbo la Moshi Vijijini, kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), bado unafukuta. Anaandika Yusuph Katimba … (endelea).

Safari hii, tuhuma zinaelekezwa moja kwa moja kwa Philemon Ndesamburo, mwenyekiti wa Chadema mkoani Kilimanjaro na Salum Mwalimu, naibu katibu mkuu wa chama hicho (Zanzibar).

Wote wawili wanatuhumiwa kuvuruga uchaguzi huo kwa maslahi binafsi.

Ndesamburo anatuhumiwa kumwaga mamilioni ya shilingi kwa lengo la kulainisha wajumbe ili wamchague mwanawe, Lucy Owenya, ambaye ni mtoto wake wa kumzaa. Kwa sasa, Owenya ni mbunge wa Viti Maalum (Chadema), kupitia mkoa wa Kilimanjaro.

Ndesamburo, mfanyabiashara maarufu nchini na mbunge wa Moshi Mjini (Chadema), anatuhumiwa kutumia zaidi ya Sh. 50 milioni kuhonga wapigakura. Anadaiwa kuwasomba baadhi yao kwa magari kutoka jimboni Moshi Vijijini na kuwalipia huduma za chakula na malazi mjini Moshi.

Taarifa kamili itawajia hivi punde.

error: Content is protected !!