October 1, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Ndege yaanguka, 107 wahofiwa kufa

Spread the love

HABIRIA 107 waliokuwa ndani Airbus A320, ndege ya Shirika la Ndega la Pakistan, wanahofia kufariki dunia baada ya ndege hiyo kuangua Karachi, Pakistan ikitokea Lahore. Inaripoti mitandao ya kimataifa … (endelea).

Sehemu ndege hiyo ilipoangukia, ilikuwa ikifuka moshi mkubwa. Ndege hiyo imenguka saa saba mchana leo tarehe 22 Mei 2020.

“Ndege yetu imeanguka Karachi. Tunajaribu kuwasiliana ili kuwa na uthibitisho idadi kamili ya watu waliokuwemo kwenye ndege hiyo.

“… lakini taarifa za awali zinaeleza, kulikuwa na abiria 99 na wahudumu wanane,” amesema Abdul Sattar Khokhar, msemaji wa mamlaka za ndege Pakistan na kuongeza “hatujawa na taarifa zaidi ya kisa hicho.”

Ndege hiyo imeanguka ikiwa ni siku chache tangu serikali ya Pakistani kuanza kuruhusi ndege za kibiashara kurejea kazini, baada ya wiki kadhaa kufungwa ili kupunguza maambukizi ya virusi vya corona.

Mpaka sasa, taarifa zaidi hazijapatikana ikiwa ni pamoja na uchunguzi wa awali.

error: Content is protected !!