January 23, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Ndege yaanguka na kuua 150

Ndege kama hii ndiyo iliyoanguka

Spread the love

NDEGE ya Airbus A320 ya Germanwings, kampuni tanzu ya Lufthansa ya Ujerumani imeanguka huko kwenye safu za milima ya Ufaransa leo Jumanne na kuua watu 150. Hii ni ajali mbaya ya ndege kutokea kwa kipindi cha karne 4 huko Ufaransa.

Waziri wa sheria wa Ufaransa amesema hamna mtu aliyesalimika, huko kwenye safu za milima ya Ufaransa sehemu ambayo ni ngumu kuweza kufikia kwa gari, na hivyo itawalazimu kutUmia Helikopta. 

Mamlaka ya mawasiliano ya anga ilisema ilipoteza mawasilinao na ndege hiyo iliyobeba abiria 144 na wafanyakazi wa ndege 6, baada ya kupata taarifa ya tatizo kwenye ndege hiyo, taarifa iliyotumwa saa 4.30 za asubuhi leo kwa muda wa Ufaransa.

Taarifa hiyo ya hali isiyokuwa ya kawaida ilitumwa na kuonyesha ndege ilikuwa angani  umbali wa futi 5,000. 

Ajali mbaya zaidi kutokea Ufaransa ni ile ya ndege ya Uturuki ya mwaka 1974 iliyoua watu 346; mwaka  1981 ndege nyingine ilianguka kwenye visiwa vya Corsica  na kuua watu 180; July 2000 France Concorde ilianguka muda mfupi baada ya kuruka ikiwa inaelekea New York, ajali hii iliyositisha huduma za ndege aina ya Concorde mpaka leo hazindelea kutoa huduma.

Mpaka sasa ajali mbaya zaidi kutokea Duniani ni ile ya 1977 watu 583 walipoteza maisha baada ya ndege mbili za Boeing 747 kugongana kwenye njia za kurukia zikiwa uwanjani visiwa vya Canary huko Uhispania. Ajali nyingine ni ile ya 1985 wakati Boeing 747 ya shirika la ndege la Japan iliangamiza watu 520 

error: Content is protected !!