Sunday , 19 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Ndege ya Precision ‘yaanguka’ Bukoba
Habari MchanganyikoTangulizi

Ndege ya Precision ‘yaanguka’ Bukoba

Ndege ya Precision ikiwa imezama katika ziwa Victoria baada ya kushindwa kutua uwanja wa Ndege wa Bukoba, Kagera
Spread the love

 

NDEGE ya kampuni ya Precision kutoka Tanzania, iliyokuwa ikisafiri kutoka Dar es Salaam, kuelekea Bukoba, imepata hitilafu na kulazimika kutua majini mjini Bukoba. Anaripoti Saed Kubenea, Bukoba … (endelea).

Taarifa zilizothibitishwa na mmoja wa wafanyakazi wa ndege hiyo zinasema, hitilafu hiyo, ilitokana na ndege hiyo, kushindwa kutoa matairi wakati wa kutua katika uwanja wa Ndege wa Bukoba, majira ya saa tatu asubuhi ya leo Jumapili, 6 Novemba 2022.

Anasema, “ni kweli kwamba ndege yetu iliyokuwa ikitokea Dar es Salaam kuja Bukoba, imepata hitilafu na rubani kulazimika kufanya kinachoitwa, ‘emergence landing’ – kutua kwa dharura majini, mita chache kutoka uwanja wa ndege wa Bukoba Mjini.”

Anaogeza, “lakini tunashukuru Mungu, hii ilikuwa ni technical issue (tatizo la kiufundi). Hivyo tushuruku kwamba baadhi ya abiria waliokuwamo kwenye ndege hiyo, mpaka sasa, tayari wameokolewa. Mengine yataelezwa na kampuni na serikali baada ya kupatikana taarifa zote zinazotakiwa.”

Kwa mujibu wa taarifa hizo, ndege yenye namba za usajili, ATR 42, yenye namba 5HPWF, namba ya mruko PW494, iliyokuwa inaendeshwa na kampteni Rwegalu Rubaga akisaidiwa na Peter Omondi.

Ilikuwa na abiria 39, wafanyakazi wawili na marubani wawili.

Mfanyakazi huyo ambaye hakupenda kutajwa jina lake, kwa kuwa si msemaji wa kampuni hiyo, anamshukuru rubani ya ndege hiyo ambaye hakumtaja jina kwa jitihada zake za kuokoa maisha ya abiria waliokuwamo ndani ya ndege.

Shirika la ndege la Precision Air, ni moja ya makampuni ya ndege binafsi makubwa nchini yenye makao yake makuu jijini Dar es Salaam, ikitajwa kufanya safari zake katika maeneo mbalimbali nchini na nchi jirani.

Inahudumia maelfu ya watalii, wananchi wa kawaida na wafanyabiashara wanaosafiri kati ya viwanja vya ndege 10 nchini Tanzania, pamoja na Nairobi na Mombasa, nchini Kenya, Entebbe (Uganda) na Johannesburg (Afrika Kusini).

Maeneo mengine inayofanya safari zake, ni Arusha, Kigoma, Kilimanjaro, Musoma, Mwanza, Bukoba, Shinyanga, Tabora, Zanzibar.

Makao yake makuu ni kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, mjini Dar es Salaam na vituo viko kwenye viwanja vya ndege vya Kilimanjaro, Arusha na Mwanza.

Kampuni ya Precision Air ilianzishwa mwaka 1991 na Mtanzania anayefahamika kwa jina la Ngaleku Shirima, na kwamba ilianza kutoa huduma zake mwaka 1994. Wakati inaanzishwa ilikuwa kampuni binafsi kwa asilimia mia moja.

Hata hivyo, baadaye shirika la ndege la Kenya Airways, lilinunua asilimia 49ya hisa za Precision Air kwa thamani ya dola za Marekani 2 milioni.

Ununuzi huu, ulifanyika wiki chache baada ya shirika la ndege la Afrika Kusini – South African Airways (SAA), kununua 49 asilimia za hisa na shirika la ndege la Tanzania, Air Tanzania Corporation (ATC).

Kuanzia Oktoba 2011, Precision Air iliamua kuanza kuuza hisa zake katika soko la hisa la Dar es Salaam na hivyo umiliki wa Michael Shirima na Kenya Airways utapungua mpaka asilimia 33 kila mmoja.

Baada ya kuanza kuuza hisa zake kwa umma, Michael Shirima alitoa nusu ya hisa zake na Kenya Airways wakatoa nusu ya hisa zao.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

CCM yamteua Pele kuwa mgombea ubunge Kwahani

Spread the loveKamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Canada yatenga bilioni 38 kutekeleza mradi ya kuinua vijana TZ

Spread the loveSERIKALI ya Canada kupitia ‘CARE International Canada’ imetenga takribani Sh...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Ujenzi kituo cha kupoza umeme Chalinze wafikia asilimia 93.7

Spread the loveKamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imeeleza...

Habari Mchanganyiko

Balile ateuliwa rais wa wahariri Afrika Mashariki

Spread the loveJumuiya ya Wahariri wa Afrika Mashariki (EAES), imemchagua Mwenyekiti wa...

error: Content is protected !!