
Wachezaji wa Mtibwa Sugar wakishangilia moja ya mabao yao waliyofunga katika mchezo wao dhidi ya Yanga
WAGENI wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Ndanda FC wameanzia kileleni kufuatia ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya wenyeji Stand United Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.
Ndanda imekaa kileleni kutokana na kuwa na idadi kubwa ya mabao zaidi ya timu nyingine ambazo zimeshinda katika michezo ya jana.
Nafasi ya pili inashikiliwa na Azam FC ambao waliibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya wageni wengine kwenye ligi hiyo, Polisi Morogoro mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi.
[pullquote]
MATOKEO MECHI ZA UFUNGUZI LIGI KUU YA VODACOM TZ BARA LEO
Azam FC 3-1 Polisi Moro
Stand Utd 1-4 Ndanda FC
Mgambo 1-0 Kagera Sugar
Ruvu Shooting 0-2 Prisons
Mtibwa Sugar 2-0 Yanga
Mbeya City 0-0 JKT Ruvu
[/pullquote]
Mtibwa Sugar iliyoifunga mabao 2-0 Yanga SC Uwanja wa Jamhuri, Morogoro ipo nafasi ya tatu sawa na Prisons ya Mbeya iliyowachapa wenyeji Ruvu Shooting mabao 2-0, wakati JKT Mgambo 1-0 iliyoilaza Kagera Sugar 1-0 ipo chini yao.
Mbeya City iliyolazimishwa sare ya 0-0 na JKT Ruvu Uwanja wa Sokoine, Mbeya iko juu ya Yanga SC iliyolala 2-0 na timu nyingine zote zilizopoteza mechi leo.
Ligi Kuu itaendelea leo katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakati Coastal Union ya Tanga itakuwa wageni wa Simba SC. Katika mchezo huo Simba wanaweza kumkosa mshambuliaji wake, Emmanuel Okwi ambaye bado hana kibali cha kufanya kazi nchini.
Kocha wa Simba, Patrick Phiri amesema hana wasiwasi kukosekana kwa Okwi kwani anaamini safu yake ya ushambuliaji itaongozwa na Raphael Kiongera na Amissi Tambwe na watafanya kazi nzuri kuipa ushindi timu yake.
More Stories
La Chaaz yateketea
Pikipiki 16 zakamtwa Dar, 10 mbaroni
Magufuli aomba wimbo wa Prof Jay, acheza